Pata taarifa kuu

Kenya yaondoa marufuku ya kutembea usiku

Nchini Kenya, rais Uhuru Kenyatta, ametangaza kuondoa masharti ya watu kutotoka nje kati ya saa nne usiku na saa kumi Alfajiri, masharti ambayo yamekuwa yakitekelezwa tangu mwezi Machi mwaka 2020 wakati, maambukizi ya virusi vya Corona yalivyoripotiwa nchini humo.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta. Ludovic MARIN AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kwenye sherehe za kuadhimisha sikukuu ya mashujaa, kiongozi huyo wa Kenya amesema uamuzi huu umekuja baada ya kupungua kwa maambukizi ya virusi nchini humo.

Hatua hii imekuja baada ya Kenya kuripoti maambukizi zaidi ya Laki 250 na vifo zaidi ya Elfu tano, wakati huu asimilia 4.6 ya watu nchini humo wakiwa wamepata chanjo kamili ya kupambana na maambukizi ya Corona.

Katika hatua nyingine, rais wa Malawi Lazarus Chakwera amekuwa mgeni rasmi kwenye maadhmo ya sikukuu ya Mashujaa, kuwakumbuka watu waliopigania uhuru na wale waliofanya mambo makubwa kwa ajili ya nchi hiyo tangu mwaka 1963.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.