Pata taarifa kuu
UGANDA-USHIRIKIANO

Uganda yapokea watu 51 kutoka Afghanistan

Ndege ya kwanza kutoka Afghanistan imetua Jumatano hii Agosti 25 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe nchini Uganda. Watu 51 wamepokelewa nchini humo kwa muda na watu wengi zaidi wanaohamishwa wanatarajia kuwasili nchini Uganda katika siku zijazo.

Picha ya video inayoonyesha msafara uliobeba kundi la kwanza la raia wa Afghanistan waliondolewa nchini humo na kupelekwa Uganda njiani wakitoka uwanja wa ndege
Picha ya video inayoonyesha msafara uliobeba kundi la kwanza la raia wa Afghanistan waliondolewa nchini humo na kupelekwa Uganda njiani wakitoka uwanja wa ndege AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla, mabasi matatu yaliyozungukwa na msafara wa polisi, yamewabeba watu 51 waliondolewa kutoka Afghanistan ambao wamewasili leo Jumatano asubuhi nchini Uganda. Wakimbizi wa Afghanistan kwa upande mmoja na watu wengine kutoka mataifa mbalimbali wamepewa hifadhi katika hoteli moja, karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa Entebbe. Viongozi wa Uganda na Marekani wamekuwa wakijadili kwa zaidi ya wiki moja kuhusiana na mapokezi ya raia hao.

Ndege zingine kutoka Kabul zinatarajiwa kuwasili nhini Uganda katika siku zijazo. Kwa jumla, karibu watu 2,000 wanatarajiwa kupewa hifadhi kwa muda nchini Uganda, kabla ya kutumwa katika nchi zingine, ikiwa ni pamoja na Marekani. Mamlaka ya Uganda imekubali kupokea raia hao kutoka Uganda kwa ombi la viongozi wa Marekani.

Lakini wakati huo huo, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje, baadhi ya raia wa Uganda ambao bado wamekwama nchini Afghanistan bado hawajaweza kuondolewa kwa sababu ya ugumu wa kufika katika uwanja wa ndege wa Kabul. Wizara imesema iko inajiandaa kuwawezesha kuchukua ndege katika siku zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.