Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Biden ahakikisha Agosti 31 kuwa tarehe ya mwisho ya kuondoka Afghanistan

Rais wa Marekani Joe Biden amesema Marekani iko mbioni kuhakikisha kuwa inawaondoa Wamarekani na watu wengine ambao maisha yao yapo hatarini kutoka nchini Afganistan kufikia tarehe 31 mwezi Agosti, licha ya shinikizo kutoka Umoja wa Ulaya (EU), kutaka asogeze mbele tarehe hiyo.

Rais wa Marekani Joe Biden katika Ikulu ya White Agosti 23, 2021.
Rais wa Marekani Joe Biden katika Ikulu ya White Agosti 23, 2021. Getty Images via AFP - DREW ANGERER
Matangazo ya kibiashara

Biden amesema mpaka sasa watu zaidi ya Elfu 70 wameshandolewa mjini Kabul tangu wapiganaji wa Taliban walipochukua udhibiti wa nchi hiyo.

Taliban tayari wameonya kuwa hawataruhusu wanajeshi wa Marekani kuendelea kuwa nchini humo zaidi ya mwisho wa mwezi huu, uongozi wa Taliban ukiwataka watu wenye fani kama Udaktari kutoondoka nchini humo.

Hayoyanajiri wakati inadaiwa kuwa mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) alikutana kisiri kwa mazungumzo na kiongozi wa Taliban huko Kabul Jumatatu wiki hii. Vyanzo vimeviambia vyombo vya habari vya Marekani kuwa CIA hawajathibitisha mkutano huo ulioripotiwa kati ya William Burns na Mullah Baradar.

Vyanzo vimeambia vituo vya habari vya Marekani , pamoja na New York Times, Washington Post, Associated Press na NPR juu ya mkutano wa CIA na Taliban.

Gazeti la Washington Post linasema majadiliano hayo yanaweza kuwa yamehusisha tarehe ya mwisho ya jeshi la Marekani kumaliza operesheni yake ya kuwaondoa watu nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.