Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

RSF yamuomba Joe Biden kufikiria kuwaokoa waandishi wa habari wa Afghanistan

Shirika la kimataifa la Waandishi Wasiokuwa na Mipaka (RSF) wametolea wito rais wa Marekani Joe Biden kufikiria " mpango maalum wa kuwaondoa waandishi wa habari wa Afghanistan," kulingana na taarifa ya shirika hilo ambayo shirika la habari la  AFP limepata kopi.

Mikusanyiko imefanyika katika miji kadhaa kote nchini kupinga Taliban. Lakini wasiwasi unaongezeka haraka miongoni mwa raia.
Mikusanyiko imefanyika katika miji kadhaa kote nchini kupinga Taliban. Lakini wasiwasi unaongezeka haraka miongoni mwa raia. AP - Rahmat Gul
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati rais wa Marekani Joe Biden anatarajia kulihutubia taifa Jumamosi hii, Agosti 21. Hii ni mara ya pili kwa siku chache kuzungumza kuhusiana na zoezi hili na operesheni zinazoendana.

Awali rais wa Marekani Joe Biden aliapa kuwa atawarejesha nyumbani raia wote wa Marekani kutoka nchini Afghanistan pamoja na Waafghani waliosaidia juhudi za nchi yake kwenye vita vya karibu miaka 20

Biden ametoa ahadi hiyo alipozungumza na waandishi habari mjini Washington wakati hatma ya maelfu ya Wamarekani waliokwama kwenye uwanja wa ndege mjini Kabul bado haijulikani. Hadi kufikia sasa ni watu 5,700 pekee ikiwemo Wamarekani 250 ndiyo wameondoshwa nchini Afghanistan na kupelekwa kwenye vituo vya muda vilivyoandaliwa kwenye mataifa jirani.

Miongoni mwa wale wanaotaka kuitoroka Afghanistan kwa kuhofia usalama wao ni Gohar, kijana anayefanya kazi katika kituo cha redio katika mkoa wa Kunar, mashariki mwa nchi. Hajaondoka nyumbani kwake kwa siku kadhaa, na ni mmoja wa watu walio katika hatari zaidi kwa sasa.

"Ninafanya kazi katika kituo cha redio, na katika makala yangu, ninatolea wito watu kutunza amani, kutokubali maadui wa amani. Nasema Taliban sio nzuri kwa Afghanistan. Najua kuna vituo vya redio vinavyorusha matangazo katika baadhi ya mikoa kwa niaba ya Taliban, lakini katika maeneo hayo ni hatari zaidi kwetu. Kwa sababu kila mtu ananijua katika mkoa wangu, Wataliban wanajua jina langu, kwamba ninafanya kazi kwa redio hii, ”anasema Gohar.

Kijana huyo anaelezea kuwa kituo chake cha redio hakirushi tena matangazo yake, kwa sababu hakuna wafanyakazi, wote wamekimbia. Na jambo jingine ni kwamba Taliban sasa inakataza kucheza muziki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.