Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Wasiwasi waongezeka miongoni mwa raia waliokwama Afghanistan

Nchini Afghanistan, zoezi la kuhamisha raia wa kigeni linaendelea na Waafghani wengi wanataka kuondoka nchini. Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi, NATO, imetoa wito kwa Taliban kuruhusu kuondoka watu wanaotaka kuondoka nchini humo.

Waandamanaji wa Afghanistan wanashilia bendera ya taifa siku ya Uhuru wa Afghanistan Agosti 19, 2021 huko Kabul.
Waandamanaji wa Afghanistan wanashilia bendera ya taifa siku ya Uhuru wa Afghanistan Agosti 19, 2021 huko Kabul. AFP - WAKIL KOHSAR
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, mikusanyiko imefanyika katika miji kadhaa kote nchini kupinga Taliban. Lakini wasiwasi unaongezeka haraka miongoni mwa raia.

Hayo yanajiri wakati rais wa Marekani Joe Biden anatarajia kulihutubia taifa Jumamosi hii, Agosti 21. Hii ni mara ya pili kwa siku chache kuzungumza kuhusiana na zoezi hili na operesheni zinazoendana.

Miongoni mwa wale wanaotaka kuitoroka Afghanistan ni Gohar, kijana anayefanya kazi katika kituo cha redio katika mkoawa Kunar, mashariki mwa nchi. Hajaondoka nyumbani kwake kwa siku kadhaa, na ni mmoja wa watu walio katika hatari zaidi kwa sasa.

"Ninafanya kazi katika kituo cha redio, na katika makala yangu, ninatolea wito watu kutunza amani, kutokubali maadui wa amani. Nasema Taliban sio nzuri kwa Afghanistan. Najua kuna vituo vya redio vinavyorusha matangazo katika baadhi ya mikoa kwa niaba ya Taliban, lakini katika maeneo hayo ni hatari zaidi kwetu. Kwa sababu kila mtu ananijua katika mkoa wangu, Wataliban wanajua jina langu, kwamba ninafanya kazi kwa redio hii, ”anasema Gohar.

Kijana huyo anaelezea kuwa kituo chake cha redio hakirushi tena matangazo yake, kwa sababu hakuna wafanyakazi, wote wamekimbia. Na jambo jingine ni kwamba Taliban sasa inakataza kucheza muziki.

Biden aapa kuwaondoa raia wake Afghanistan

Awali rais wa Marekani Joe Biden aliapa kuwa atawarejesha nyumbani raia wote wa Marekani kutoka nchini Afghanistan pamoja na Waafghani waliosaidia juhudi za nchi yake kwenye vita vya karibu miaka 20

Biden ametoa ahadi hiyo alipozungumza na waandishi habari mjini Washington wakati hatma ya maelfu ya Wamarekani waliokwama kwenye uwanja wa ndege mjini Kabul bado haijulikani. Hadi kufikia sasa ni watu 5,700 pekee ikiwemo Wamarekani 250 ndiyo wameondoshwa nchini Afghanistan na kupelekwa kwenye vituo vya muda vilivyoandaliwa kwenye mataifa jirani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.