Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: Kundi la upinzani dhidi ya Taliban lajiimarisha Panchir

Siku chache baada ya Afghanistan kuangka mikononi mwa Taliban, upinzani dhidi ya kundi hilo umeanza kujidhatiti katika eneo la Panchir, Kaskazini Mashariki mwa Afghanistan.

Wapiganaji wa Taliban wakitazama bendera yao Kabul, agost 17, 2021.
Wapiganaji wa Taliban wakitazama bendera yao Kabul, agost 17, 2021. Hoshang Hashimi AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Moscow, uasi umeanza kujimarisha katika eneo la Panchir, uasi ambao umeanzishwa na makamu wa rais wa zamani wa Afghanistan Amrullah Saleh na mtoto wa aliyekuwa mpinzani mkuu wa Taliban hayati kamanda Massoud.

"Wataliban hawadhibiti nchi yote ya Afghanistan", amebainisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov katika mkutano na waandishi wa habari huko Moscow.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov ametoa wito wa mazungumzo kwa lengo la kuunda "serikali ya umoja" nchini Afghanistan.

Makamu wa rais wa zamani wa Afghanistan Amrullah Saleh ameapa kutojisalimisha mbele ya Taliban na amamuwa kuanzisha vita vya maguguni dhidi ya kundi hilo kwenye Bonde la Panchir.

Siku ya Jumatatu, picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilimwonyesha akiwa pamoja na Ahmad Massoud,  katikajimbo hilo, wakionekana kuweka jiwe la msingi la kuanzisha vuguvugu la wapinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.