Pata taarifa kuu

Israeli imefungua tena mpaka wa Kerem Shalom kuruhusu misaada kuingia Gaza

Jeshi la Israeli limethibitisha kufungua tena mpaka wa Kerem Shalom unaoingia katika ukanda wa Gaza baada ya kufungwa awali.

Mamlaka nchini Israeli ilifunga mpaka huo wa Kerem Shalom baada ya wapiganaji wa Hamas kurusha makombora nchini mwaka.
Mamlaka nchini Israeli ilifunga mpaka huo wa Kerem Shalom baada ya wapiganaji wa Hamas kurusha makombora nchini mwaka. REUTERS - TYRONE SIU
Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya misaada yanaeleza kuwa mpaka huo ambao ulifungwa wikendi iliopita baada ya shambulio la roketi la Hamas kuwauwa wanajeshi wanne wa Israeli ni muhimu kwa ajili ya kuwasilisha misaada kwa waathiriwa wa mapigano katika ukanda wa Gaza.

Zaidi ya raia milioni moja wa Palestina wanapokea hifadhi katika eneo la Rafah baada ya kutoroka mapigano katika maeneo mengine.
Zaidi ya raia milioni moja wa Palestina wanapokea hifadhi katika eneo la Rafah baada ya kutoroka mapigano katika maeneo mengine. AP - Hatem Ali

Hatua hii inakuja wakati wanajeshi wa Israel sasa wakisema wanadhibiti eneo la mpaka muhimu kuingia kwenye mji wa Rafah, hatua ambayo Marekani inasema ni operesheni ya kawaida ambayo haikuwa na madhara, licha ya onyo linaloendelea kutolewa na jumuiya ya kimataifa kuhusu Operesheni yoyote ya Israel kwenye mji huo.

Aidha katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameonya kuhusu misaada kutofika kwa raia wa Palestina ikiwa mipaka ya Rafah itafungwa.

“Natoa wito kwa pande zote kuonyesha ukomavu wa kisiasa na kupata mkataba wa kusitisha vita sasa na kuacha umawaji damu na kuachia huru mateka. ’’ Alisema katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.

00:44

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa

Washirika wa Israeli wamekuwa wakionya dhidi ya oparesheni zake katika eneo la Rafah lenye idadi ya raia wa Palestina zadi ya milioni moja wengi wao ambao walitoroka mapigano yanayoendelea kati ya Hamas na wanajeshi wa Israeli katika maeneo mengine.

Israeli inasisitiza kuwa Rafah ndio eneo peke ambalo wapiganaji wa Hamas wangali wanajificha na kwamba inahitaji kumaliza kundi hilo na washirika wake.

Israeli iliwataka wakaazi wa Rafah kuondoka katika eneo hilo kuelekea oparesheni zake za kijeshi.
Israeli iliwataka wakaazi wa Rafah kuondoka katika eneo hilo kuelekea oparesheni zake za kijeshi. © Ramadan Abed / Reuters

Marekani ilisitisha mpango wake wa kutuma mabomu nchini Israeli wiki iliopita kutokana na hofu kuwa mshirika wake alikuwa anakaribia kutekeleza oparesheni za kijeshi katika eneo la Rafah.

Haya yanajiri wakati huu ujumbe wa Hamas na ule wa Serikali ya Israeli ukikutana Misri, kujaribu kukamilisha makubaliano ya usitishaji mapigano baada ya Hamas kuridhia.

Soma piaIsraeli imetuma magari kivita kwenye eneo la Rafah katika ukanda wa Gaza

Marekani, Misri na nchi yake Qatar ambao ni wapatanishi wakuu katika mzozo wa Hamas na Israeli wanaendelea na juhudi zao za kuafikia suluhu ya usitishaji wa mapigano katika ukanda wa Gaza.

Mpaka wa Rafah umekuwa muhimu kwa mashirika ya kutoa misaada tangu mapigano kuzuka na ndilo eneo peke ambalo raia wanaweza kuingia na kuondoka Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.