Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: Rais Ashraf Ghani ahutubia taifa kutoka Abu Dhabi

Kwa mara ya kwanza tangu mji mkuu wa Afghanistan, Kabu,l kuangukia mikononi mwa Taliban, rais aliyetimuliwa mamlakani Ashraf Ghani alizungumza, Jumatano, Agosti 18, kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu alikopata hifadhi ya ukimbizi.

Rais wa zamani wa Afghanistan Ashraf Ghani akilihutubia taifa kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu, ambapo alipokelewa baada ya Taliban kuchukua madaraka Agosti 18, 2021.
Rais wa zamani wa Afghanistan Ashraf Ghani akilihutubia taifa kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu, ambapo alipokelewa baada ya Taliban kuchukua madaraka Agosti 18, 2021. - AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake kwa taifa, rais aliyeondolewa mamlakani amekiri kushindwa kisiasa na kijeshi dhidi ya Taliban, ambao wameanzisha mazungumzo na viongozi wa zamani wa Afghanistan. Rais wa zamani Hamid Karzai alikutana wa mazungumzo na kiongozi kutoka kundi hilo, Anas Haqqani.

Ashraf Ghani alionekana peke yake mbele ya kamera, akiwa amevaa shati jeupe na koti jeusi, bendera ya Afghanistan ikiwa nyuma yake, ameripoti Vincent Souriau mwandisi wetu huko Dubai. "Ilibidi nikimbilie katika Umoja wa Falme za Kiarabu kwa sababu walitaka kuninyonga hadharani," amebaini Ashraf Ghani. Mapema leo, serikali ilitangaza kuwa iko tayari kuwapokea "kwa sababu za kibinadamu" rais huyo wa zamani na familia yake.

"Kushindwa huku ni kwetu na kwa washirika wetu wa kimataifa"

Ashraf Ghani anadai kuwa "aliondoka nchini kwa kuzuia damu nyingi zisimwagiki na uharibifu wa mji wa Kabul". “Ndio, ni tumeshindwa, lakini tumeshindwa sote, serikali yetu, na washirika wetu wa kimataifa, sote tumeshindwa dhidi ya vita vya Taliban. Kwa sababu kile kilichoanza kama mchakato wa amani kimemalizika kama vita, " amebaini Ashraf Ghani.

"Sasa lazima tujadili, na ninaunga mkono mazungumzo yaliyoanzishwa na Taliban na rais wa zamani Hamid Karzai. Lakini mimi, sintochoka. Ninajadili jinsi ya kurudi nyumbani Afghanistan, ambapo ninataendelea kupigania haki na maadili yetu, "ameongeza Ashraf Ghani.

Lakini, wakati Taliban wamerudi madarakani, ushawishi wa Ghani umeshuka. Siku ya Jumatano Marekani ilibaini kwamba rais huyo wa zamani "sio mtu tena wa kutegemea nchini Afghanistan."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.