Pata taarifa kuu

Waelfu ya watu waendelea kuutoroka mji wa Rafah kufuatia mashambulizi ya jeshi la Israel

Maelfu ya Wapalestina wanaoishi kwenye mji wa Rafah wenye wakaazi zaidi ya Milioni 1.5, wameendelea kukimbilia maeneo mengine, wakati huu  jeshi la Israel likitekeleza mashambulio, licha ya pingamizi kutoka kwenye Jumuiya ya Kimataifa.

Wapalestina waliokimbia makazi yao wamewasili katikati mwa Gaza baada ya kutoroka Rafah kusini. Deir al-Balah, Alhamisi Mei 9, 2024.
Wapalestina waliokimbia makazi yao wamewasili katikati mwa Gaza baada ya kutoroka Rafah kusini. Deir al-Balah, Alhamisi Mei 9, 2024. AP - Abdel Kareem Hana
Matangazo ya kibiashara

Wakati hayo yakijiri, rais wa Marekani Joe Biden, amesema serikali yake haitatoa msaada wa silaha kwa Israeli kutekeleza mashambulio kwenye mji wa Rafah, iwapo vikosi vya ardhini vitaanza operesheni kwenye mji huo.

Licha ya shinikizo za kimataifa zinazoongozwa na Marekani, kujaribu kuizuia Israel kutekeleza mashalbulio hayo yanayohofiwa kuwa, yatakuwa na madhara makubwa hasa kwa rais, wiki hii Israel ilituma magari ya kuvita, katika êneo la mpaka wa mji wa Rafah na Misri.

Katika hatua nyingine,  Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya kibinadamu imesema jeshi la Israeli limefunga tena mpaka wa Rafah, hali ambayo inazuia misaada ya kibinadamu kuwafikia wakaazi wa Gaza.

Israel imeendelea kusisitiza kuwa itaendelea na operesheni yake mjini Rafah, huku kundi la Hamas likiishtumu Israel kwa kuanza mashambulio ili kuzuia mazungumzo ya kutafuta suluhu ya vita vinavyoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.