Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Wachambuzi : Ushindi wa Taliban katika vita Afghanistan utaimarisha ugaidi

Baada ya wapiganaji wa Taliban kuchukua udhibiti wa Afghanistan, wachambuzi wa mambo wanaonya kuwa hatua hii inawapa nguvu majihadi wa Kiisamu duniani.

Msemaji wa kundi la Taliban Zabihullah Mujahidkatika mkutano na waanishi wa habari, Kabul.
Msemaji wa kundi la Taliban Zabihullah Mujahidkatika mkutano na waanishi wa habari, Kabul. Hoshang HASHIMI AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya Taliban kuchukua udhibiti wa Afghanistan, kwa wachambuzi wa masuala ya siasa na usalama, ni kama kuyaamisha makundi ya kijihadi kuwa yanaweza kupambana na kuyaondoa majeshi ya kigeni kama Marekani.

Colin Clarke,mtafiti kutoka shirika la Soufan Centre nchini Marekani, anaona kuwa, dunia itarajie propanda kutoka kwa makundi hayo ya kijihadi zinazolenga kuwatia moyo wapiganaji hao hasa Kaskazini mwa Afrika na Kusini Mashariki mwa bara Asia.

Aymenn Jawad Al-Tamimi mtafiti wa harakati za kijihadi, kutoka Chuo Kikuu cha George Washington naye anaona kuwa, uvumilivu ulioneshwa na Taliban, utakuwa ni ujumbe kwa makundi hayo ya kijihadi kuendelea kupambana ili vikosi vya kigeni vinavyopambana nao katika nchi mbalimbali, viondoke.

Licha ya kutofautiana kiaidolojia na Taliban, kundi kama Islamic State linatarajiwa kutumia kuanguka kwa serikali ya Afganistan, kama eneo salama la kuendeleza harakati zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.