Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Taliban yafanya msako dhidi ya maadui zake wa zamani

Baada ya kuchukua madaraka nchini Afghanistan siku ya Jumapili Agosti 15, Taliban wamesema wanataka kuanzisha serikali ya umoja, itakayovumulia wapinzani wake. Hawana "nia ya kulipiza kisasi," amesema msemaji wa Taliban. Lakini, papo hapo, hali ni tofauti na yale aliyotamka.

Wapiganaji wa Taliban huko Kunduz, mapema Agosti 2021 (picha ya kumbukumbu).
Wapiganaji wa Taliban huko Kunduz, mapema Agosti 2021 (picha ya kumbukumbu). AP - Abdullah Sahil
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa, wapiganaji wakundi hilo wameanzisha msako ili kupata maadui wake wa zamani. Kwa kuongezea, uhaba wa chakula unaendelea kuongezeka nchini.

Taliban wanadaiwa kuwa wana "orodha za watu inayosaka" ambao wanataka kuwakamata, kulingana na Umoja wa Mataifa. Hawa ni maafisa wa zamani wa Afghanistan na wanajeshi. Wote walifanya kazi au kushirikiana na vikosi vya Marekani na NATO katika mapigano. Ili kuzipata, Wataliban wanafanya msako wa nyumba kwa nyumba. Wanaenda moja kwa moja kwenye nyumba za wale wanaolengwa na hawasiti kutishia wanafamilia wao ikiwa watakataa kujisalimisha.

Wakati mwingine hata huchukua hatua: wiki iliyopita, miili kadhaa ya wanajeshi wa zamani wa Afghanistan walipatikana huko Kandahar, kusini mwa nchi. Karibu wengine 10,000 wanaaminika kuwa mafichoni, limeripoti Gazeti la New York Times. Makabila na dini zenye wa umini wa chache nchini, pia, wnaripotiwa kulengwa na Taliban. Wanaume tisa kutoka jamii ya Washia Hazara waliteswa na kuuawa na wapiganaji wa Talibani, shirika la Haki z Binadamu, la Amnesty International limesema. Hali hiyo ilitokea mwanzoni mwa mwezi Julai, katika mkoa wa Ghazni, masharikiwa Afghanistan.

Kwa upande wao, waandishi wa habari hawaokolewi.Jamaa wa mwandishi wa habari kutoka Deutsche Welle, mtangazaji wa umma wa Ujerumani, amekutwa amekufa. Wiki hii, Taliban iliteka nyara nyumba za "angalau waandishi wa habari wanne na wafanyikazi wa vyombo vya habari," kulingana na Kamati ya Kulinda Wanahabari. Wengine wawili walipigwa huko Jalalabad.

Uhaba wa chakula

Kwa kuongezea, ukosefu wa chakula nchini Afghanistan, kwa sababu ya athari za pamoja za vita nchini na matokeo ya ongezeko la joto duniani, unaendelea kuongezeka, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani limebaini. "Mmoja kati ya Waafghanistan watatu," anasema Kun Li, msemaji wa WFP - anayewakilisha watu milioni 14 - ni ukosefu wa chakula na watoto milioni mbili wanaugua utapiamlo na wanahitaji matibabu ya haraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.