Pata taarifa kuu

Misri-Israel: Cairo yatia wasiwasi na vifaru vya Israel karibu na mpaka wa Misri na Gaza

Mvutano umeongezeka kati ya Misri na Israel kufuatia kuwasili kwa magari ya kivita ya Israel karibu na mpaka wa Misri na Gaza, eneo linaloitwa "Philadelphia Corridor."

Vifaru vya usafiri wa wanajeshi wa Misri vikipiga kambi karibu na kivuko cha Rafah, Machi 23, 2024. Mvutano unaongezeka kati ya Misri na Israeli karibu na "Philadelphia Corridor".
Vifaru vya usafiri wa wanajeshi wa Misri vikipiga kambi karibu na kivuko cha Rafah, Machi 23, 2024. Mvutano unaongezeka kati ya Misri na Israeli karibu na "Philadelphia Corridor". AFP - KHALED DESOUKI
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Misri, Alexandre Buccianti

Makubaliano ya "Philadelphia Corridor" yalihitimishwa mwaka 2005 kufuatia Israel kujiondoa kwa upande mmoja kutoka Ukanda wa Gaza. Chini ya mkataba huu wa amani, eneo lisilo na jeshi ambalo lilikuwa linapita kwenye mpaka wa upande unaokaliwa na Israeli lilikuwa katka makubaliano.

Walinzi wa mpaka 750 wa Misri

Upande wa Misri wa Corridor ulikabidhiwa kwa walinzi wa mpaka 750 waliotumwa na Cairo. Na upande wa Palestina ulidhibitiwa na Mamlaka ya Palestina. Tangu mwaka 2007, baada ya Hamas kutwaa Gaza, Misri imekuwa doria katika ukanda peke yake. Mnamo mwezi wa Desemba 2023 Israeli ilitangaza kwamba inataka kuchukua udhibiti wa upande wa Palestina wa "ukanda" huu "kuzuia upitishaji wa silaha kwa Hamas kutoka Misri".

"Kuongezeka kwa mvutano"

Cairo ilikuwa imekataa rasmi. Kulingana na vyanzo vilivyo karibu na idara ya ujasusi, Misri, kufuatia kuwasili kwa magari ya kivita kwenye corridor, "imeonya Israeli juu ya uzito wa kuongezeka kwa uhsama kwenye mpaka na kubaii kwamba maswali yote yalikuwa mezani" bila kutoa maelezo zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.