Pata taarifa kuu

Biden awasihi Wamarekani kutoa mabilioni ya msaada kwa Israeli na Ukraine

Kwa mara ya pili tu katika muhula wake, Joe Biden amehutubia raia wake kutoka ikulu ya White House akiwataka kutoa msaad kwa kwa Israel na Ukraine. Hotuba iliyotajwa kuwa kuu na Ikulu ya White House. Hili ni ombi la Joe Biden kwa msaada wa Marekani kwa Ukraine na Israel.

Rais wa Marekani Joe Biden amehutubia taifa kutetea sera ya nje ya Marekani nchini Ukraine na vita vya Hamas na Israel.
Rais wa Marekani Joe Biden amehutubia taifa kutetea sera ya nje ya Marekani nchini Ukraine na vita vya Hamas na Israel. Getty Images via AFP - POOL
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Washington, Guillaume Naudin

Hotuba ya rais Biden imedumu robo saa tu. Dakika kumi na tano fupi kwa rais kuelezea kwa nini anaomba Baraza la Congress Ijumaa hii kwa msaada wa dharura kwa Israeli na Ukraine, amsaada ambao unaweza kuzidi dola bilioni 100 kwa mwaka mmoja.

Rais Joe Biden anasema, nchi hizo mbili zinakabiliwa na wavamizi, Hamas na Urusi, ambao wanataka kuharibu demokrasia kwa nchi mbili. Anakataa kuruhusu hili kutokea, na anasema kwamba ikiwa Marekani haiungi mkono Israeli na Ukraine, basi gharama itakuwa kubwa zaidi. Anakumbusha kwamba Vladimir Putin na viongozi wa Urusi tayari wametishia Poland na nchi za Baltic, washirika wa NATO. Pia anasisitiza kuwa Hamas haiwawakilishi Wapalestina ambao pia wana haki ya kuishi kwa amani na usalama sawa na majirani zao wa Israel.

Kwa mara nyingine tena amewataka Waisrael kujizuia na hasira zao na kuheshimu sheria za kibinadamu katika kukabiliana na Hamas. Joe Biden pia amesema ana wasiwasi kuhusu matokeo ya mzozo wa Mashariki ya Kati nchini Marekani. Ameonya dhidi ya chuki kwa Wayahudi na Uislamu. Kwa sababu hii ni hotuba ya kisiasa ya ndani. Na ameimbaa kwamba mgawanyiko mkubwa wa kisiasa nchini na katika barazala la Congress usidhoofishe Marekani, ambayo anaichukulia kama taifa muhimu na kinara wa dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.