Pata taarifa kuu

Hamas: Msaada wa Marekani kwa Israel ni sawa na 'uchokozi' dhidi ya Wapalestina

Kuimarishwa kwa msaada wa kijeshi kwa Israel uliotangazwa na Washington kusaidia nchi hiyo kukabiliana na mashambulizi yaliyoanzishwa na Hamas ni sawa na "kushiriki katika uchokozi dhidi ya raia wetu", Hamas, chama cha wanamgambo wenye itikadi kali walio madarakani huko Gaza kimetangaza siku ya Jumapili, Oktoba 8. 

Wanajeshi wa Israeli waliotumwa Sderot, Oktoba 7, 2023.
Wanajeshi wa Israeli waliotumwa Sderot, Oktoba 7, 2023. AP - Ohad Zwigenberg
Matangazo ya kibiashara

"Tangazo la Marekani (la msaada wa ziada wa kijeshi wa Marekani kwa Israel) ni ushiriki wa kweli katika uchokozi dhidi ya raia wetu," imesema taarifa ya Hamas. "Vitendo hivi haviwatishi watu wetu wala harakati ambazo ztaendelea kuwatetea," Hamas imeongeza katika taarifa yake.

Rais wa Marekani Joe Biden ameagiza "msaada ziada" kutoka Marekani kwa Israel, kufuatia mashambulizi ambayo hayajawahi kufanywa na Hamas kutoka Ukanda wa Gaza, Ikulu ya White House imesemasiku ya  Jumapili, Oktoba 8.

Katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Jumapili, rais Joe Biden ametangaza kwamba "msaada wa ziada kwa wanajeshi wa Israel sasa uko njiani kuelekea Israel, na mengine zaidi yatafuata katika siku zijazo," kulingana na taarifa ya Ikulu ya White House.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.