Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Hezbollah yadai kuhusika na mashambulizi dhidi ya Israel kutoka Lebanon

Hezbollah imesema katika taarifa Jumapili kwamba imeshambulia maeneo matatu ya Israel katika eneo linalozozaniwa kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili kwa kutumia "idadi kubwa ya makombora ya mizinga." Imeongeza kuwa imerusha makombora hayo "kwa mshikamano na upinzani na watu wa Palestina" siku moja baada ya mashambulizi makubwa yaliyoanzishwa na Hamas dhidi ya Israel kutoka Ukanda wa Gaza.

Mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel ukizuia makombora yaliyorushwa kutoka Ukanda wa Gaza, katika eneo la Ashkelon, Oktoba 8, 2023.
Mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel ukizuia makombora yaliyorushwa kutoka Ukanda wa Gaza, katika eneo la Ashkelon, Oktoba 8, 2023. © AMIR COHEN / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Israel na Ukanda wa Gaza wako vitani. Tangu kuanzishwa kwa shambulio la Hamas nchini Israel Jumamosi asubuhi, ghasia hizo zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 300 na 1,864 kujeruhiwa kwa upande wa Israeli, vyombo vya habari vya Israeli vimeripoti Jumapili asubuhi.

Kundi hilo limesema katika taarifa kwamba shambulio hilo limelenga vituo  vitatu, ikiwa ni pamoja na "eneo la rada" katika Mashamba ya Chebaa, shamba linalokaliwa na Israel tangu 1967 na ambalo Lebanon inadai kuwa ni eneo lake.

Vikosi vya Israel vimeshambulia kusini mwa Lebanon siku ya Jumapili kujibu mashambulizi kutoka eneo hili, jeshi la Israeli limesema katika taarifa iliyochapishwa muda mfupi kabla ya 7:30 asubuhi Jumapili. "Vikosi vya Israel vinashambulia eneo la Lebanon ambako hutokea makombora hayo," taarifa hiyo imesema.

Mapigano ya ardhini

Wakati wa usiku kuanzia Jumamosi hadi Jumapili, mapigano ya ardhini kati ya wanajeshi wa Israel na "mamia" ya wapiganaji waliojipenyeza yaliendelea hadi usiku katika "maeneo 22," kulingana na msemaji wa jeshi la Israeli. Wavamizi hawa waliwateka nyara Waisraeli kadhaa siku ya Jumamosi, idadi ambayo bado haijafahamika. Msemaji huyo alitaja tu "hali mbaya inayowakabili mateka" ndani ya eneo la kilomita 20 mashariki mwa Ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.