Pata taarifa kuu

Rais wa Marekani Joe Biden aagiza 'msaada wa ziada' kwa Israel

Rais wa Marekani Joe Biden ameagiza "msaada ziada" kutoka Marekani kwa Israel, kufuatia mashambulizi ambayo hayajawahi kufanywa na Hamas kutoka Ukanda wa Gaza, Ikulu ya White House imesemasiku ya  Jumapili, Oktoba 8.

Rais wa Marekani Joe Biden, akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, anazungumza kuhusu mzozo wa Israel, baada ya Hamas kuanzisha mashambulizi yake makubwa zaidi katika miongo kadhaa, wakati akitoa taarifa kuhusu mgogoro huo, katika Ikulu ya White House mjini Washington, Marekani Oktoba 7, 2023.
Rais wa Marekani Joe Biden, akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, anazungumza kuhusu mzozo wa Israel, baada ya Hamas kuanzisha mashambulizi yake makubwa zaidi katika miongo kadhaa, wakati akitoa taarifa kuhusu mgogoro huo, katika Ikulu ya White House mjini Washington, Marekani Oktoba 7, 2023. REUTERS - ELIZABETH FRANTZ
Matangazo ya kibiashara

Marekani imeanza kutuma msaada wa kijeshi kwa Israel na silaha mpya siku ya Jumapili, na kuisogeza meli yake kubwa ya kikosi cha wanamaji na angani karibu na Bahari ya Mediterania, kuashiria uungaji mkono wa haraka kwa mshirika wake wa kihistoria kufuatia mashambulizi ya Hamas kutoka Palestina.

Katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Jumapili, rais Joe Biden ametangaza kwamba "msaada wa ziada kwa wanajeshi wa Israel sasa uko njiani kuelekea Israel, na mengine zaidi yatafuata katika siku zijazo," kulingana na taarifa ya Ikulu ya White House.

"Rais ameagiza uungwaji mkono zaidi kwa Israel kufuatia shambulio la kigaidi la Hamas ambalo halijawahi kushuhudiwa," serikali ya Marekani imesema katika taarifa yake fupi. Matangazo maalum zaidi yanawezakutolewa baadaye, Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken alisema hapo awali.

Kifurushi cha kwanza cha msaada wa kijeshi "kitaanza kusafirishwa leo na kitawasili siku zijazo," Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema katika taarifa yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.