Pata taarifa kuu

Marekani kuweka vikwazo kwa uzalishaji wa hewa chafu kwa mitambo ya nishati ya makaa ya mawe

Serikali ya Joe Biden imetangaza hivi punde siku ya Alhamisi kwamba itaweka vikwazo vikali kwa uzalishaji wa CO2 kutoka kwa mitambo ya nishati ya makaa ya mawe kuanzia mwaka 2032 kupanga kuendelea kufanya kazi kwa muda mrefu, hatua ambayo inapaswa kusaidia Marekani kufikia ahadi zake za tabianchi.

Kiwanda cha kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe cha BP huko Gelsenkirchen, Ujerumani, Alhamisi, Januari 16, 2020. (picha ya kielelezo)
Kiwanda cha kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe cha BP huko Gelsenkirchen, Ujerumani, Alhamisi, Januari 16, 2020. (picha ya kielelezo) AP - Martin Meissner
Matangazo ya kibiashara

Udhibiti huu mpya, ambao pia unahusu mitambo ya kuzalisha nishati ya gesi itakayojengwa siku za usoni, unatokana na teknolojia ya kunasa kaboni, ambayo bado ni nadra sana na ya gharama kubwa.

Haya ni matangazo "makubwa" ambayo "yanatusogeza mbele katika mapambano yetu dhidi ya mzozo wa tabianchi," ametangaza Ali Zaidi, mshauri wa rais Joe Biden katika masuala ya tabianchi. "Sekta ya nishati sasa ina zana nyingi za kupunguza uchafuzi wake kuliko hapo awali."

Uzalishaji wa umeme unawakilisha karibu robo ya uzalishaji wa gesi chafu nchini, sekta ya pili kwa ukubwa baada ya usafiri.

Chini ya sheria mpya, mitambo ya nishati ya makaa ya mawe ambayo inapanga kuendelea kufanya kazi baada ya mwaka 2039 italazimika kunasa 90% ya uzalishaji wao wa CO2, kuanzia mwaka 2032.

Mitambpo inayopanga kufunga ifikapo 2039 - karibu nusu ya vinu vya nishati ya makaa ya mawe nchini, kulingana na serikali - watalazimika kunasa 16% ya uzalishaji wao ifikapo mwaka 2030. Hatimaye, ile iliyopumziswa kabla ya mwaka 2032 haina kikomo chochote.

Mitambo mipya ya nishati ya gesi inayofanya kazi kwa kiwango cha juu pia italazimika kuwa na vifaa vya kunasa 90% ya CO2 yao ifikapo mwaka 2032.

Kanuni hizo zilipendekezwa mwaka mmoja uliopita na shirika la Ulinzi wa Mazingira la Marekani (EPA), na baada ya mashauriano ya lazima ya umma, sasa zimekamilika -- lakini bila ya mabadiliko kadhaa.

Kanuni za mwisho hazijumuishi tena mitambo iliyopo ya nguvu ya gesi, ambayo lazima sasa iwe chini ya kiwango tofauti. Na tarehe ambayo mitambo ya nishati ya makaa ya mawe italazimika kunasa 90% ya CO2 yao imerudishwa nyuma kutoka mwaka 2030 hadi 2032.

- "Ni jambo la kihistoria" -

Hadi sasa, hakukuwa na viwango vya shirikisho vinavyozuia uzalishaji kutoka kwa mitambo iliyopo ya nishati ya makaa ya mawe. Hata hivyo, hizi zinawakilisha chanzo kikubwa zaidi cha uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwa sekta ya nishati, kulingana na EPA.

Kanuni zinapaswa kuzuia utoaji wa karibu tani bilioni 1.4 za CO2 ifikapo mwaka 2047, sawa na utoaji wa kila mwaka wa magari milioni 328, imesema EPA.

Kiwango hiki ni mojawapo ya "zana zenye ufanisi zaidi kuwahi kutengenezwa ili kupunguza uzalishaji unaoharibu hali ya hewa kutoka kwa sekta ya nishati," limejibu shirika la Sierra Club.

"Ni ya kihistoria", serikali ya Joe Biden "itakuwa imefanya zaidi ya utawala mwingine wowote" kwa hali ya hewa, Margie Alt, mkurugenzi wa "Climate action campaign", muungano unaoleta pamoja karibu mashirika kumi ya mazingira.

Hakuna teknolojia iliyowekwa kwa makampuni ili kufikia malengo ya kupunguza uzalishaji, lakini EPA inapendekeza kuwa chaguo bora litakuwa kunasa na kuhifadhi CO2 (CCS), ambayo inaruhusu kunaswa badala ya kutolewa angani.

Hata hivyo, kwa sasa kuna takriban maeneo 40 pekee ya kunasa CO2 duniani kwa michakato ya kiviwanda au uzalishaji wa umeme, kulingana na Shirika la Nishati la Kimataifa.

Kwa mujibu wa shirika la 350.org, teknolojia hizi bado hazijathibitisha wenyewe, na ni badala ya idadi ya vinu hivi ambavyo inapaswa kupunguzwa.

"Wawakilishi wa makampuni kadhaa ya umeme wameonyesha kuwa CCS ni teknolojia inayoweza kutumika kwa sekta ya nishati leo," hata hivyo amehakikisha mkuu wa EPA, Michael Regan, akikumbusha mikopo ya kodi iliyotolewa kwa mbinu hizi na sheria ya hivi karibuni ya hali ya hewa (IRA).

- Kanuni "zinazokithiri" -

Kulingana na Mwakilishi wa Texas Republican Chip Roy, EPA "inaua uzalishaji wa umeme unaotegemewa." Kundi la America's Power, ambalo linawakilisha tasnia ya makaa ya mawe, limeta kiwango kipya "kilichokithiri na haramu."

Kiwango hiki kinaweza kupingwa mahakamani, na Donald Trump alikuwa tayari ametangaza nia yake ya kutafakari upya iwapo atachaguliwa kuwa rais mwezi Novemba.

EPA pia ilitangaza siku ya Alhamisi kanuni nyingine tatu kuhusu mitambo ya nishati ya makaa ya mawe, ili kupunguza utoaji wao wa metali zenye sumu (zebaki, nikeli, n.k.), uchafuzi wa umwagaji wao kwenye maji na majivu ya makaa ya mawe.

Idadi kubwa ya mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe imefungwa katika muongo mmoja uliopita nchini Marekani. Wakati huo huo, uzalishaji wa umeme kupitia nishati ya jua na upepo, lakini pia ya mitambo ya nguvu ya gesi, imeongezeka.

Mnamo mwaka 2023, karibu 60% ya uzalishaji wa umeme wa Marekani ulitoka kwa gesi (43%) au makaa ya mawe (16%), kulingana na shirika la Marekani kuhusu Taarifa ya Nishati, ikifuatiwa na nishati mbadala ( 21%), na nyuklia (18%).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.