Pata taarifa kuu

Takriban watu 80 waangamia katika mkasa wa moto Hawaii, mamlaka yashushiwa lawama

Takriban watu 80 wamefariki kutokana na moto ambao umeteketeza kisiwa cha Maui, Hawaii, hali ambayo imesababisha mamlaka kukosolewa kutokana na jinsi walivyoshughulikia mojawapo ya maafa mabaya zaidi ya asili katika historia ya hivi majuzi ya Visiwa vya Marekani.

Raia huyu anatembelea mabaki ya nyumba yake, iliyoharibiwa na moto huko Lahaina, Agosti 11, 2023.
Raia huyu anatembelea mabaki ya nyumba yake, iliyoharibiwa na moto huko Lahaina, Agosti 11, 2023. © Rick Bowmer / AP
Matangazo ya kibiashara

Wakazi , wakiwa bado na mshtuko, ndio kwanza wanaanza kuona uharibifu uliotokea Lahaina, mji ambao karibu utetketezwe wote kwa moto huo.

Vikosi vya uokoaji vinaendelea na kazi kwenye magofu yanayofuka moshi katika eneo la Lahaina. 

Hayo yanajiri wakati moto mwingine uliozuka kwenye kisiwa hicho usiku wa kuamkia leo umelazimisha mamia ya watu kuhamishwa na kupelekwa eneo la kaskazini mashariki ambalo nalo liliungua mwanzoni mwa wiki hii.

Mkasa huo wa moto unatajwa kuwa ndiyo janga baya zaidi la asili katika historia ya kisiwa hicho, ukilipiku janga la tsunami lililosababisha vifo vya watu 61 mnamo mwaka 1960, takribani mwaka mmoja baada ya Hawaii kujiunga na Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.