Pata taarifa kuu

Marekani: Mkasa wa moto ni 'janga kubwa zaidi la asili katika historia ya Hawaii'

"Hili ni janga kubwa zaidi la asili katika historia ya Hawaii," Gavana wa jimbo hilo Josh Green amesema. Idadi ya vifo kutokana na moto katika kisiwa cha Maui imefikia angalau 67, lakini zoezi la utafutaji linaendelea na idadi hiyo inaweza kuongezeka zaidi.

Mji wa Lahaina uliteketea baada ya moto kuzuka huko Hawaii, Agosti 10, 2023.
Mji wa Lahaina uliteketea baada ya moto kuzuka huko Hawaii, Agosti 10, 2023. © Rick Bowmer / AP
Matangazo ya kibiashara

Mji wa Lahaina ni rundo la majivu, majengo yaliyo kuwa mbele ya bahari yote yameteketea kwa moto. Kituo cha kihistoria kimeharibiwa kabisa. Ni katika eneo hili, magharibi mwa kisiwa cha Maui ambako zoezi la utafutaji umejikita kutafuta manusura baada ya moto ulioteketeza kisiwa cha Maui katika Bahari ya Pasifiki. Ni vigumu kutoa ripoti ya uhakika: mamlaka inakadiria idadi ya waliotoweka kwa maelfu, lakini ni wangapi kati yao wamefariki? Ni vigumu kusema kwa vile mawasiliano ni magumu katika sehemu za kisiwa ambazo hazina umeme na simu hazifanyi kazi kwa sasa.

"Nadhani idadi ya watu waliofariki inaweza kuongezeka zaidi, kwa sababu miili iliyopatikana ni ya watu waliogunduliwa nje ya majengo yaliyoteketezwa kwa moto," meya wa kisiwa hicho, Richard Bissen, alisema Ijumaa Agosti 11. Bado hatujaweza kufikia ndani ya majengo hayo, tunasubiri kuwasili kwa usaidizi kutoka kwa shirika la shirikisho la Marekani lililobobea katika hali za dharura (FEMA) lililo na vifaa maalumu vya kutosha kwa shughuli hizi.

"Kwa sasa, tunajikita na watu waliopotea. Tunataka kuleta pamoja familia. Tunataka kumpa kila mtu habari: kujua ikiwa wako kwenye makazi ya muda au ikiwa ni miongoni mwa waliofariki. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.