Pata taarifa kuu

Baada ya Marekani, Mexico pia yakabiliwa na baridi kali ya kipekee

Wimbi la baridi nchini Marekani linaenea hadi Mexico, ambapo hali ya baridi kali isiyo ya kawaida ya hadi -15 ° C inatarajiwa. Mikoa ya milima kaskazini mwa nchi imeathirika zaidi, pamoja na Mexico ya kati, ambapo maporomoko ya theluji ya kipekee yameonekana.

Wahamiaji wanajaribu kupata joto dhidi ya wimbi la baridi linaloikumba Amerika Kaskazini baada ya kulala nje usiku, kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico, huko El Paso, karibu na Texas, Desemba 22, 2022.
Wahamiaji wanajaribu kupata joto dhidi ya wimbi la baridi linaloikumba Amerika Kaskazini baada ya kulala nje usiku, kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico, huko El Paso, karibu na Texas, Desemba 22, 2022. © John Moore / Getty Images via AFP
Matangazo ya kibiashara

Dhoruba 'kali ya baridi' kya kipekee. Hivi ndivyo Mexico inavyotaja viwango vya baridi vya chini visivyo kuwa vya kawaida ambavyo vinaathiri ameneo ya kaskazini na katikati mwa nchi, hadi mji mkuu.

Dhoruba kali ya baridi ambayo imeikumba Marekani katika siku za hivi karibuni inaenea kwa jirani yake ya kusini, ambayo haijajiandaa vyema kukabiliana na hali hizi mbaya. Katika maeneo ya milimani yaliyo mashariki mwa Jiji la Mexico, theluji imeanguka, jambo ambalo ni nadra sana kutokea nchini humo.

Hali ya kaskazini mwa nchi ni mbaya zaidi: -15°C hadi -10°C, mafuriko na dhoruba kali ya baridi vimetangazwa leo Jumatano, Desemba 28.

Wahamiaji wameathirika sana

Nyumba nyingi za Mexico hazina mfumo wa joto, lakini mamlaka pia ina wasiwasi kuhusu wahamiaji kupiga kambi karibu na mpaka na Marekani. Licha ya baridi kali, makundi haya ya wahamiaji kutoka Amerika ya Kati na Venezuela yameazimia kukaa na kujaribu kujipasha moto karibu na moto ulioboreshwa.

Kwa wiki kadhaa, wamekuwa wakingoja kuweza kuwasilisha ombi la hifadhi kwa upande mwingine wa vikwazo, matarajio yanayozidi kutokuwa na uhakika

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.