Pata taarifa kuu

Mexico yawasilisha malalamiko kwa ICJ kufuatia shambulio dhidi ya ubalozi wake Quito

Mexico imewasilisha malalamiko dhidi ya Ecuador kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) siku ya Alhamisi, baada ya polisi kufanya shambulio dhidi ya ubalozi wake huko Quito ambalo lilisababisha kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili na kuzua hasira katika jumuiya ya kimataifa.

Polisi na wanajeshi wakiwa mbele ya ubalozi wa Mexico mjini Quito, Aprili 5, 2024.
Polisi na wanajeshi wakiwa mbele ya ubalozi wa Mexico mjini Quito, Aprili 5, 2024. REUTERS - Karen Toro
Matangazo ya kibiashara

Katika malalamiko yake, Mexico inaomba Ecuador isimamishwe katika Umoja wa Mataifa "hadi itaomba msamaha hadharani, kwa kutambua ukiukwaji wa kanuni za msingi na kanuni za sheria za kimataifa", Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico Alicia Barcelona alitangaza Alhamisi, Aprili 11 wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Lengo ni "kudhamini fidia kwa uharibifu wa maadili kwa taifa la Mexico na raia wake", alisisitiza waziri. Ni lazima tuzuie kitendo kama hicho "kurudiwa" mahali pengine ulimwenguni, alisema Rais Andrés Manuel López Obrador.

Naibu wa balozi alidhulumiwa wakati wa uingiliaji kati wa watu wenye silaha usiku wa Aprili 5, ambao ulitokea baada ya mfululizo wa matukio yaliyoelezwa kama "vitendo vya vitisho" kama vile kurekodiwa kwa maongezi ya simu na kuwafukuza wafanyakazi. Sehemu hii ya utaratibu juu ya uhalali inaweza kuchukua miaka kadhaa, anasisitiza mwandishi wetu huko Hague, Stéphanie Maupas. Wakati huo huo, Mexico inaomba majaji kuagiza- haraka iwezekanavyo - Ecuador kulinda majengo yake ya kidiplomasia, pamoja na mali na kumbukumbu yanahifadhiwa katikamajengo yake nchii Ecuador. Na kuzuia uingiliaji wowote. Quito pia imeombwa kuwezesha "kusafisha kwa majengo", pamoja na nyumba za kibinafsi za wawakilishi wake. Majibu ya waamuzi yanatarajiwa kutolewa haraka.

Jorge Glas kwenye alengwa

Polisi waliingia katika ubalozi wa Mexico huko Quito mnamo Aprili 5 kumkamata makamu wa rais wa zamani wa Ecuador anayetuhumiwa kwa ufisadi, Jorge Glas, ambaye alikuwa amekimbilia katika ubalozi wa Mexico, Quito.

Mexico ilitangaza mara moja kusitishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia na Ecuador na mara moja ikasema nia yake ya kudai mbele ya ICJ asili isiyoweza kukiukwa ya uwakilishi wa kidiplomasia, iliyoanzishwa na Mkataba wa Vienna wa 1961.

Kwa upande wake, Rais wa Ecuador Daniel Noboa alitetea uvamizi wa ubalozi kama inavyohitajika ili kumkamata Jorge Glas kwa sababu aliwasilisha "hatari ya kutoroka", akisema yuko tayari "kusuluhisha mzozo wowote" na Mexico. Akituhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma zilizokusudiwa kujenga upya miji ya pwani baada ya tetemeko la ardhi mnamo mwaka 2016 na kushiriki katika mfumo wa ufisadi wa kampuni ya ujenzi ya Odebrecht ya Brazil, Jorge Glas alihukumiwa mwaka wa 2017 kifungo cha miaka minane gerezani. Aliachiliwa mnamo mwaka 2022 kutokana na rufaa ya kisheria, kisha akakimbilia mwezi Desemba 2023 katika ubalozi wa Mexico huko Quito, kabla ya kupata hifadhi ya kisiasa.

Jorge Glas (picha ya zamani ya mwaka 2019), aliyekuwa makamu wa rais wa Ecuador.
Jorge Glas (picha ya zamani ya mwaka 2019), aliyekuwa makamu wa rais wa Ecuador. AFP

Mshirika wa karibu wa rais wa zamani Rafael Correa, alipelekwa Jumatatu katika hospitali ya wanamaji huko Guayaquil, kusini magharibi mwa Ecuador. Ripoti ya polisi inataja matumizi ya kupita kiasi ya dawa za kuhangaisha na kupunguza msongo wa mawazo ambayo yalimtumbukiza kwenye kukosa fahamu. Siku iliyofuata, alirudi kwenye gereza lenye ulinzi mkali huko Guayaquil. Rafael Correa alihakikisha Jumatano kwamba Jorge Glas, 54, alikuwa kwenye mgomo wa kula. "Hakula chochote na aligoma kula," alisema kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Rafael Correa, ambaye aliongoza Ecuador kutoka mwaka 2007 hadi mwaka 2017, alihukumiwa bila kuwepo kwa kifungo cha miaka minane kwa rushwa na anaishi uhamishoni nchini Ubelgiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.