Pata taarifa kuu

Lebanon Kusini: Wanajeshi watatu wa UN na Mlebanon mmoja wajeruhiwa katika mlipuko

Waangalizi watatu wa kijeshi wa Umoja wa Mataifa na msaidizi wa raia wa Lebanon wamejeruhiwa siku ya Jumamosi, Machi 30, kusini mwa Lebanon, inayokumbwa na mapigano makali kati ya Hezbollah na jeshi la Israel tangu Oktoba 8, kufuatia vita vya Gaza.

Mwanajeshi wa UNIFIL nchini Lebanon.
Mwanajeshi wa UNIFIL nchini Lebanon. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mazingira ya mkasa huu uliootokea katika kijiji cha mpakani cha Rmeich hayajulikani. Jeshi la Lebanon limetangaza kuwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wamejeruhiwa wakati gari lao lilipopigwa na ndege isio na rubani ya Israel, madai ambayo taifa la Kiyahudi limekanusha mara moja.

Msemaji wa Kikosi cha Muda cha Umoja wa Mataifa, UNIFIL, kilichotumwa kusini mwa nchi hiyo, Andrea Tenenti, ametangaza kwa upande wake kwamba mlipuko ulitokea karibu na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa waliokuwa wakishika doria ya Kundi la waangalizi nchini Lebanon. Chombo hiki cha Umoja wa Mataifa kina jukumu la kufuatilia usuluhishi uliohitimishwa kati ya Lebanon na Israeli mnamo mwaka 1949 na hufanya kazi kwa karibu na UNIFIL.

Hili si tukio la kwanza kuwahusisha wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon. Mnamo Novemba 25, 2023, UNIFIL ilitangaza kwamba moja ya doria zake iilishambuliwa na Israeli bila kusababisha hasara yoyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.