Pata taarifa kuu

Vita vya Israel na Hamas: Antony Blinken kuzuru Mashariki ya Kati kuepusha mgogoro wa kikanda

Mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken anaanza Alhamisi, Januari 4, ziara nyingine huko Mashariki ya Kati kwa matumaini ya kuepuka upanuzi wa vita huko Gaza baada ya kuaawa naibu kiongozi wa Hamas nchini Lebanon na milipuko mibaya iliyoikumbwa Iran siku ya Jumatano Alaasiri.

Wanajeshi wa Israeli wakirusha kombora kutoka kusini mwa Israeli kuelekea Ukanda wa Gaza, Jumatano Januari 3, 2024.
Wanajeshi wa Israeli wakirusha kombora kutoka kusini mwa Israeli kuelekea Ukanda wa Gaza, Jumatano Januari 3, 2024. AP - Leo Correa
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ataanza ziara nyingine ya kidiplomasia huko Mashariki ya Kati leo Alhamisi jioni, ikiwa ni ziara ya nne tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas, huku akitarajiwa kuzuru Israel, afisa wa Marekani alisema siku ya Jumatano jioni.

Kifo cha naibu kiongozi wa Hamas, Saleh al-Arouri, aliyeuawa katika shambulizi la siku ya Jumanne, kimeongeza zaidi hofu kwamba Mashariki ya Kati nzima itakumwa na vitaa. Siku ya Jumatano Hassan Nasrallah, kiongozi wa Hezbollah, alisema kwamba kundi lake "halitakaa kimya" baada ya "uchokozi huu wa wazi wa Israel" huko Beirut.

Wakati wa hotuba iliyosubiriwa kwa hamu siku ya Jumatano Januari 3, katibu mkuu wa Hezbollah alihakikisha kwamba kuuawa kwa naibu kiongozi wa Hamas, Saleh el-Arouri, wakati wa shambulizi la anga - la Israel - siku ya Jumanne jioni, "halitabaki bila kuadhibiwa."

Jeshi la Israel liliendelea na mashambulizi yake ya anga katika Ukanda wa Gaza usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi, hasa huko Khan Younes (kusini) na Deir al-Balah (katikati), ambapo Wizara ya Afya ya Hamas imeripoti fifo vingine.

Kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa siku ya Jumatano Januari 3 na Wizara ya Afya ya Hamas, watu 22,313 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Watu karibu 60,000 walijeruhiwa. Jeshi la Israel limedai leo Alhamisi kuwa limewaua zaidi ya wapiganaji 2,000 wa Kipalestina tangu kumalizika kwa mapatano ya usitishwaji wa mapigano mapema mwezi Desemba. Wanajeshi 175 wa Israel wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya ardhini ya jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza Oktoba 27, kulingana na takwimu za hivi punde za jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.