Pata taarifa kuu

Hofu ya vita vya kamili yaongezeka kufuatia kifo cha naibu kiongozi wa Hamas nchini Lebanon

Wakati wa hotuba iliyotarajiwa sana Jumatano Januari 3, katibu mkuu wa Hezbollah allihakikisha kwamba kuuawa kwa naibu kiongozi wa Hamas, Saleh el-Arouri, wakati wa shambulizi la anga - la Israel - Jumanne jioni, "hakutabaki bila kuadhibiwa."

Jengo ambalo Hamas naibu kiongozi wa Hamas alikuwemo lililolengwa na shambulizi la anga mnamo Jumanne Januari 2, 2024, huko Beirut.
Jengo ambalo Hamas naibu kiongozi wa Hamas alikuwemo lililolengwa na shambulizi la anga mnamo Jumanne Januari 2, 2024, huko Beirut. AP - Bilal Hussein
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Beirut, Paul Khalifeh

"Kwa sasa, tunapigana kwenye uwanja wa vita kwa hesabu [...] lakini ikiwa adui anafikiria kuanzisha vita dhidi ya Lebanon, tutapigana bila kikomo," alisema Hassan Nasarallah, kiongozi wa Hezbollah kundi lenye nguvu nchini Lebanon, katika hotuba iliyosubiriwa kwa hamu siku ya Jumatano jioni, baada ya kifo cha Saleh el-Arouri.

Jambo ambalo linalifanya Gazeti la kila siku la Annahar kusema kwamba "hatari za mzozo wa kimataifa kati ya Lebanon na Israeli hazijawahi kuwa karibu sana". Mhariri wa Gazeti la Al-Akhbar, lililo na ukaribu na Hezbollah, anadai kwamba silaha zitakazotumiwa na Hezbollah katika vita vinavyowezekana "hazitakuwa za kawaida." Wasiwasi huo huo pia uko miongoni mwa baadhi ya wanasiasa, ambao wamelaani shambulio la anga lililomuua Saleh Al-Arouri,huku wakielezea hofu yao ya kuona Lebanon ikiingizwa kwenye vita kamili.

Shinikizo kwenye mpaka

Wakati huo huo, mapigano kwenye mpaka wa Lebanon na Israel yanazidi kuongezeka. Silaha zinazotumwa na wapiganaji kutooka pande mbili zinafikia hatua mpya kila siku. Hezbollah ilishambulia maeneo kadhaa ya Israeli siku ya Jumatano na makombora mazito yaliyokuwa yalibeba kilo 300 za vilipuzi. Pia ilirusha makombora na mabomu mbalimbali.

Siku ya Jumatano, ndege za Israel ziliharibu nyumba katika mji wa pwani wa Naqoura, ambao ni makao makuu ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa. Mizinga ilirusha makumi ya makombora na ndege zisizo na rubani zilianzisha mashambulizi kadhaa karibu na miji zaidi ya thelathini ya Lebanon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.