Pata taarifa kuu

Hezbollah 'haitakaa kimya' baada ya kuuawa kwa naibu kiongozi wa Hamas

Hassan Nasrallah, kiongozi wa Hezbollah, alisema katika hotuba yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu Jumatano kwamba "hawatakaa kimya" baada ya "uchokozi wa wazi wa Israel" huko Beirut.

Kiongozi wa Hezbollah, Sayyed Hassan Nasrallah akizungumza na wafuasi wake kwa njia ya video wakati wa hafla ya kuadhimisha mwaka wa nne wa mauaji ya Jenerali Qassem Soleimani, kamanda mkuu wa jeshi la Iran, katika shambulizi la Marekani, katika viunga vya kusini mwa Beirut, Lebanon, Januari 3. 2024.
Kiongozi wa Hezbollah, Sayyed Hassan Nasrallah akizungumza na wafuasi wake kwa njia ya video wakati wa hafla ya kuadhimisha mwaka wa nne wa mauaji ya Jenerali Qassem Soleimani, kamanda mkuu wa jeshi la Iran, katika shambulizi la Marekani, katika viunga vya kusini mwa Beirut, Lebanon, Januari 3. 2024. REUTERS - MOHAMED AZAKIR
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa kundi lenye nguvu la Lebanon la Hezbollah pia alisema siku ya Jumatano kwamba mauaji ya Israel ya naibu kiongozi wa kundi washirika la Hamas kutoka Palestina huko Beirut ni "uhalifu mkubwa na hatari ambao hatuwezi kunyamazia."

Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni, Sayyed Hassan Nasrallah alisema mashambulizi ya Hezbollah kuvuka mpaka dhidi ya Israel kuanzia tarehe 8 Oktoba yamezuia kampeni kubwa zaidi ya Israel ya mashambulizi ya anga, na kuionya Israel kwamba hakutakuwa na "kujizuia" na "hakuna sheria" kwa mapigano ya kundi lake ikiwa Israeli iliamua kuanzisha vita dhidi ya Lebanon.

"Nina hofu kwamba tunakaribia vita vya kikanda," Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon Abdallah Bou Habib alisema katika mahojiano kwenye CNN. "Natumai na ninafanya maombi ili kusiwepo na majibu (kutoka kwa Hezbollah). Vita vya kikanda ni mbaya kwa kila mtu. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.