Pata taarifa kuu

Israeli inasema iko tayari kwa chochote baada ya shambulio la Lebanon

Nairobi – Jeshi la Israel limesema limejitayarisha kwa tukio lolote baada ya shambulio katika mji wa Beirut nchini Lebanon ambalo limesababisha kifo cha naibu kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Hamas.

Israeli imesisitiza kuwa, kuuawa kwa naibu kiongozi huyo wa Hamas, halikuwa shambulio dhidi ya Lebanon, bali lililenga uongozi wa kundi hilo
Israeli imesisitiza kuwa, kuuawa kwa naibu kiongozi huyo wa Hamas, halikuwa shambulio dhidi ya Lebanon, bali lililenga uongozi wa kundi hilo AP - Hussein Malla
Matangazo ya kibiashara

Kumekuwa na wasiwasi kuwa, vita vinavyoendelea huenda vikasambaa na kuwa vya kikanda, iwapo vitaendelea kwa muda mrefu

Kwa mujibu wa afisa wa ngazi wa juu nchini Lebanon, al-Aruri ameuawa pamoja na walinzi wake na watu wengine sita katika shambulio hilo linalokuja baada ya Israeli kuapa kulifuta kabisa kundi la Hamas, kufutia mashambulio ya Oktoba saba mwaka uliopita Kusini mwa nchi yake.

Chanzo kingine cha usalama kimethibitisha taarifa hiyo wakati pia runinga ya Hamas ikitangaza kuwa Israeli imetekeleza mauaji ya Aruri Lebanon.

Kumekuwa na wasiwasi kuwa, vita vinavyoendelea huenda vikasambaa na kuwa vya kikanda, iwapo vitaendelea kwa muda mrefu.
Kumekuwa na wasiwasi kuwa, vita vinavyoendelea huenda vikasambaa na kuwa vya kikanda, iwapo vitaendelea kwa muda mrefu. AP - Mohammad Austaz

Israeli imesisitiza kuwa, kuuawa kwa naibu kiongozi huyo wa Hamas, halikuwa shambulio dhidi ya Lebanon, bali lililenga uongozi wa kundi hilo.

Kundi la Hamas limelaani kuuawa kwa kiongozi wake, huku kundi la Hezbollah lenye makao yake nchini Lebanon, likisema kitendo hicho cha Israeli ni kama kuivamia nchi jirani.

Kwa mujibu wa afisa wa ngazi wa juu nchini Lebanon, al-Aruri ameuawa pamoja na walinzi wake na watu wengine sita katika shambulio hil
Kwa mujibu wa afisa wa ngazi wa juu nchini Lebanon, al-Aruri ameuawa pamoja na walinzi wake na watu wengine sita katika shambulio hil REUTERS - MOHAMED AZAKIR

Kundi la Hamas na Hezbollah, zimetishia kulipiza kisasi, huku serikali ya Lebanon kupitia Waziri Mkuu wake Najib Mikati ikiilaumu Israel kwa kujairbu kuiingiza kweye vita vyake dhidi ya Hamas.

Katika hatua nyingine, jeshi la Israeli limeendelea kushambulia Gaza, na kulenga hospital katika mji wa Kusini wa Khan Younis na kuendeleza kusababisha maafa amabayo yamepita Elfu 22.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.