Pata taarifa kuu

Hezbollah yaonya kulipiza kisasi kwa 'mauaji' ya naibu kiongozi wa Hamas

Israeli haijathibitisha rasmi kuhusika katika mauaji ya naibu kiongozi wa kundi la Hamas,Saleh Al-Arouri, aliyeuawa shambulio huko Beirut siku ya Jumanne, anaripoti mwandishi wetu wa kudumu huko Jerusalem, Michel Paul. Mshauri wa Waziri Mkuu wa Israel, hata hivyo, anathibitisha kwamba "jambo moja liko wazi: hili sio shambulio dhidi ya taifa la Lebanon" lakini, kulingana na Mark Regev, "ni shambulio baya" dhidi ya uongozi wa Hamas.

Une manifestation contre le meurtre du haut responsable du Hamas, Saleh Al-Arouri, à Jénine, en Cisjordanie occupée par Israël, le 2 janvier 2024.
Maandamano ya kupinga mauaji ya afisa mkuu wa Hamas Saleh Al-Arouri huko Jenin, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel, Januari 2, 2024. © Raneen Sawafta / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amewataka wajumbe wa serikali yake kutozungumzia kifo cha Saleh Al-Arouri. Hii haikuwazuia mawaziri na wabunge kadhaa, hasa kutoka mrengo wa kulia, kuchapisha maoni kwenye mitandao ya kijamii na kukaribisha kwa uwazi mauaji yaliyolengwa ya kiongozi huyo nambari 2 wa Hamas. Dau la hatari, amebaini mwandishi/ Mhariri  asubuhi ya leo huku waandishi wengine kadhaa wakithibitisha kuwa kipindi cha kujizuia sasa kimekwisha. Maandamano ya watu wenye hasira umeandaliwa huko Aroura, karibu na Ramallah katika Ukingo wa Magharibi, kijiji cha asili cha Saleh Al-Arouri.

Nchini Israeli, hali ya tahadhari iko juu zaidi. Jeshi la Israel linasema liko tayari kwa tukio lolote baada ya shambulio katika mji wa Beirut nchini Lebanon ambalo limesababisha kifo cha naibu kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Hamas. Betri za ziada za mfumo wa ulinzi wa anga zimetumwa kaskazini mwa nchi. Hata hivyo msemaji wa jeshi Jenerali Hagari anasisitiza kuwa IDF imejikita katika mapambano dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Athari za kwanza za kuuawa kwa Saleh Al-Arouri ni kusitishwa kwa mazungumzo ya kuachiliwa kwa mateka. Na hii husababisha wasiwasi mkubwa kati ya familia zao. "Kwa vyovyote vile, tunaweza kusema asubuhi ya leo kwamba Israeli inajiandaa kwa majibu. Pamoja na swali: Ni nani atakuwa mhusika mkuu: Hamas au Hezbollah? », anamalizia mwanahabari wetu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.