Pata taarifa kuu

Lebanon: Hamas nambari 2, Saleh Al-Arouri, auawa Beirut

Kiongozi nambari mbili wa kundi la Hamas, Saleh Al-Arouri, ameuawa katika shambulio la Israeli kwenye viunga vya Beirut nchini Lebanon, siku ya Jumanne jioni, Hamas na maafisa wawili wa usalama wa Lebanon wametangaza. Hii ni mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita huko Gaza kwa Israel kuupiga mji mkuu wa Lebanon. Mapigano kati ya jeshi la Israel na Hezbollah ya Lebanon, mshirika wa Hamas ya Palestina, hadi sasa yamejikita katika maeneo ya mpakani kusini mwa Lebanon.

De gauche à droite, en partant de la ligne du haut : Mohammed Deif, Yahya Sinouar, Marwan Issa, Ismaïl Haniyeh, Khaled Mechaal, Saleh al-Arouri.
Kutoka kushoto kwenda kulia, kuanzia safu ya juu: Mohammed Deif, Yahya Sinouar, Marwan Issa, Ismaïl Haniyeh, Khaled Mechaal, Saleh al-Arouri. © AFP, AP, Wiki Commons
Matangazo ya kibiashara

Saleh Al-Arouri aliuawa pamoja na walinzi wake katika shambulio la Israel lililolenga ofisi ya Hamas katika viunga vya kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, ngome ya Hezbollah inayoiunga mkono Iran, afisa wa usalama wa Lebanon amesema. Mpiga picha wa shirika al habari la AFP aliona jengo la ghorofa mbili likidondoka na magari kuharibiwa katika eneo hilo, ambapo magari ya kubeba wagonjwa mahututi yalikuwa yakipishana.

Hamas ilithibitisha Jumanne kwamba kiongozi wake nambari mili "ameuawa" katika shambulio la Israeli huko Beirut, katika tangazo lililowasilishwa na vyombo vya habari vya kundi hilo. "Makamu wa rais wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, Sheikh Saleh Al-Arouri, amekufa shahidi katika shambulio la Wazayuni huko Beirut," Hamas imesema katika tangazo lililorushwa hewani na kituo chake rasmi, al-Aqsa TV na vyombo vyake vingine vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.