Pata taarifa kuu

Mapigano makali yarindima Gaza ambapo mzozo unaingia katika hatua mpya

Israel na Ukanda wa Gaza wameingia mwaka 2024 bila mapumziko katika mapigano. Jeshi la Israel limesema litarekebisha mbinu za vita kwa kujiondoa au kuwatuma tena baadhi ya askari wake wa akiba kuendelea na mapigano "mwaka mzima" wa 2024.

Wanajeshi wa Israeli kutoka wakijipanga katika eneo lililo karibu na mpaka wa Israel na Gaza, Januari 1, 2024.
Wanajeshi wa Israeli kutoka wakijipanga katika eneo lililo karibu na mpaka wa Israel na Gaza, Januari 1, 2024. © Leo Correa / AP
Matangazo ya kibiashara

Katika ujumbe wa mwaka mpya, msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel Daniel Hagari alisema upelekaji wa wanajeshi unarekebishwa ili kujiandaa kwa "mapigano ya muda mrefu".

Alisema baadhi ya wanajeshi, hasa askari wa akiba,wataondolewa ili kuwaruhusu kujipanga upya.

"IDF lazima ipange mapema kutokana na kuelewa kwamba kutakuwa na misheni ya ziada na mapigano yataendelea mwaka mzima." Alisema kuwa baadhi ya askari wa akiba wataondoka Gaza " wiki hii" ili kuwaruhusu "kuongeza nguvu kabla ya operesheni zinazokuja".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.