Pata taarifa kuu

Jeshi la Israeli ladai kumuua mkuu wa kitengo cha makombora cha Hezbollah nchini Lebanon

Ilikuwa ni wakati wa shambulio la anga katika eneo la Bazouriyé kusini mwa Lebanon ambapo Ali Abdel Hassan Naïm, naibu kamanda wa kitengo cha roketi na makombora cha Hezbollah aliuawa, jeshi la Israeli limebaini katika taarifa kwa vyombo vya habari. 

Gari la jeshi la Lebanon lilifunga barabara inayoelekea kwenye ghala lililoharibiwa, ambalo lilishambuliwa na mashambulizi ya anga ya Israel, nje kidogo ya kijiji cha ngome cha Hezbollah cha Buday, karibu na mji wa Baalbek, mashariki mwa Lebanon, Jumatatu, Feb. 26, 2024.
Gari la jeshi la Lebanon lilifunga barabara inayoelekea kwenye ghala lililoharibiwa, ambalo lilishambuliwa na mashambulizi ya anga ya Israel, nje kidogo ya kijiji cha ngome cha Hezbollah cha Buday, karibu na mji wa Baalbek, mashariki mwa Lebanon, Jumatatu, Feb. 26, 2024. AP - STR
Matangazo ya kibiashara

Mtu huyo "aliwajibika kwa kutekeleza na kupanga mashambulizi dhidi ya raia wa Israel," jeshi la Israeli limeongeza.

"Ndege ya Jeshi la Wanahewa la Israel limemshambulia kwa bomu na kumuua Ali Abdel Hassan Naïm, naibu kamanda wa kitengo cha roketi na makombora cha Hezbollah, katika eneo la Bazouriyé (kusini mwa Lebanon)," taarifa hiyo imesema siku ya Ijumaa Machi 29, 2024.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.