Pata taarifa kuu

Lebanon: Wapiganaji watano wa Hezbollah, akiwemo Ali al-Debs, waliuawa katika muda wa saa 24

Takriban wapiganaji watano wa Hezbollah na raia kumi na mmoja waliuawa katika muda wa saa 24 kusini mwa Lebanon katika mashambulizi ya anga ya Israel. Mamia ya wapiganaji wa chama cha Kishia waliuawa au kujeruhiwa tangu mapigano yalipoanza kwenye mpaka wa Lebanon na Israel tarehe 8 Oktoba.

Shambulio la kijeshi la Israeli kusini mwa Lebanon, likionekana kutoka kaskazini mwa Israeli, Alhamisi hii, Februari 15, 2024.
Shambulio la kijeshi la Israeli kusini mwa Lebanon, likionekana kutoka kaskazini mwa Israeli, Alhamisi hii, Februari 15, 2024. AP - Ariel Schalit
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwanahabari wetu mjini Beirut, Paul Khalifeh

Miongoni mwa wapiganaji watatu waliouawa siku ya Jumatano katika shambulizi la Israel huko Nabatieh, kusini mwa Lebanon, ni Ali al-Debs. Afisa huyu wa ngazi ya juu wa kijeshi alikuwa tayari amejeruhiwa siku chache zilizopita katika mji huo, wakati gari lake liliposhambuliwa na ndege isiyo na rubani.

Hezbollah ilitangaza kurusha makumi ya roketi dhidi ya maeneo ya Israeli huko Galilaya kujibu shambulio baya lililotekelezwa Siku ya Jumatano huko Nabatieh.

Chama cha Hassan Nasrallah tayari kimepoteza karibu wapiganaji 190, akiwemo mmoja wa viongozi wakuu wa kikosi chake cha wasomi cha al-Radwan na makamanda wawili. Takriban wapiganaji wengine 300 wa chama hicho walijeruhiwa, ikiwa ni pamoja na kadhaa vibaya, katika mashambulizi ya anga ya Israel.

Idadi hii kubwa ya waathiriwa ndani ya saa 24 inaonyesha ukubwa wa mapigano kwenye uwaja wavita katika ya Lebanon na Israeli.

Umoja wa Mataifa umetoa tahadhari dhidi ya kile ulichokiita “ongezeko hatari.”

Siku ya Alhamisi msemaji wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa waliotumwa kusini mwa Lebanon, Andrea Tenenti, ameonya kuhusu "mabadiliko yanayotia wasiwasi" katika kiwango cha uhasama mpakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.