Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Tume ya Umoja wa Ulaya yalalamikia hali ya kibinadamu Afghanistan

Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi inasema raia wengi wa Afghanistan wanaotaka kuondoka nchini humo, wanashindwa kuondoka makwao na wale ambao wanahofia maisha yao, hawana namna ya kufanya.

wapiganaji wa Taliban wanafanya msako wa nyumba kwa nyumba wakiwasaka watu waliofanya kazi na wanajeshi wa Marekani na NATO.
wapiganaji wa Taliban wanafanya msako wa nyumba kwa nyumba wakiwasaka watu waliofanya kazi na wanajeshi wa Marekani na NATO. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa UNHCR Shabia Mantoo, ametaka mataifa jirani, kuacha mipaka yao wazi, ili kuwaruhusu watu wanaokimbia nchini Afghanistan kupata makao mapya.

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP, nalo linaonya kuwa, huenda kukashuhudiwa kwa hali mbaya ya kibinadamu nchini humo, iwapo hatua za haraka hazitochukuliwa.

Wakati huo huo, ripoti za  Kiinteljensia za Umoja wa Mataifa, zikieleza kuwa, wapiganaji wa Taliban wanafanya msako wa nyumba kwa nyumba wakiwasaka watu waliofanya kazi na wanajeshi wa Marekani na NATO.

Marekani nayo inasema, mpaka sasa imefanikiwa kuwaondoa watu zaidi ya Elfu tatu kutoka jijini Kabul, kati ya watu Elfu tisa inayopanga kuwaondoa nchini humo, baada ya Taliban kuchukua udhibiti wa nchi hiyo, Agosti 14.

Ripoti zinasema, bado kuna hali ya sintofahamu katika uwanja wa Kimataifa wa ndege jijini Kabul wakati huu maelfu yta watu wanapojaribu kuondoka nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.