Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Taliban yapinga kuwahamisha "wataalam" wa Afghanistan

Msemaji wa kundi la Taliban amezitaka nchi za Magharibi ziache kuwaondoa wafanyakazi wenye ujuzi wa Afghanistan, akisema nchi hiyo inawahitaji.

Watu waliohamishwa kutoka Kabul na jeshi la Ufaransa kwenye lami uwanja wa ndege wa Al Dhafra karibu na Abu Dhabi.
Watu waliohamishwa kutoka Kabul na jeshi la Ufaransa kwenye lami uwanja wa ndege wa Al Dhafra karibu na Abu Dhabi. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Nchi za Magharibi zinapaswa kuhamisha wageni kutoka Afghanistan, sio Waafghan waliohitimu zaidi, utawala  mpya wa Taliban umeonya Jumanne (Agosti 24), huku ukikataa kusogezwa mbele kwa tarehe ya mwisho ya Agosti 31 kuhusiana na zoezi la kuaondoa raia wa kigeni na Waafghan walioshirikiana na nchi hizo kuendesha shughuli mbalimbali nchini humo.

"Wataalam, kama wahandisi, wanandolewa nchini na Marekani na washirika wao, "tunaomba waanchane na hatua hiyo", amesema mmoja wa wasemaji wa kundila Taliban Zabihullah Mujahid katika mkutano na waandishi wa habari huko Kabul, huku akibaini kwamba anapingana na hoja yoyote ya kuongeza muda wa zoezi la kuwaondoa raia wa kigeni nchini Afghanistan, badala ya tarehe 31 Agosti 2021.

"Nchi hii inahitaji utaalam wake. [Watu hawa wenye taaluma] hawapaswi kupelekwa katika nchi zingine, " amesema. Wazungu "wana ndege, wana uwanja wa ndege, wanapaswa kuchukua raia wao […] kuwapeleka nje ya nchi," Zabihullah Mujahid ameongeza. “Hawapaswi kuhimiza Waafghan kutoroka Afghanistan.

Zabihullah Mujahid ameonya kuwa hawatauruhusu Marekani kurefusha muda wa mwisho wa Agosti 31 wa kukamilisha operesheni zake za kuondoka. Rais wa Marekani Joe Biden alisema atafuata ratiba hiyo, lakini yuko chini ya shinikizo la kumtaka aombe muda zaidi kwa ajili ya uhamishwaji wa watu. 

Makumi ya maelfu ya Waafghan, wakiogopa kwamba Taliban itarejesha aina ile ile ya utawala wa kimabavu na wa kikatili kama wakati walipokuwa madarakani kati ya mwaka 1996 na 2001, wikiwa ni pamoja na wageni, wamehamishwa tangu Taliban walipochukua madaraka Agosti 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.