Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-USALAMA

Viongozi wa G7 kuijadili Afghanistan Jumanne hii

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amewaalika viongozi wa nchi zilizostawi zaidi kiuchumi G7 kwa mazungumzo ya haraka juu ya hali nchini Afghanistan.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson. JUSTIN TALLIS AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa G7 watakutana, Jumanne, Agosti 24, kujadili hali nchini Afghanistan, ametangaza Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, ambaye nchi yake kwa sasa inashikilia urais wa "kundi la nchi 7" ( Ujerumani, Canada, Marekani, Ufaransa, Italia, Japan na Uingereza).

"Jumanne nitawaalika viongozi wa G7 kwa mazungumzo ya haraka juu ya hali nchini Afghanistan. Ni muhimu kwa jamii ya kimataifa kufanya kazi pamoja kuhakikisha zoezi la kuondoa raia nchini Afghanistan linakwenda salama, kuzuia mzozo wa kibinadamu na kuwasaidia raia wa Afghanistan kulinda maendeleo (yaliyofanywa) kwa miaka 20 iliyopita, "Waziri Mkuu wa ingereza amesema kwenye ukurasa wake Twitter.

Maelfu ya Waafghan wanajaribu kuitoroka nchi yao

Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G7 ulifanyika siku ya Alhamisi. Baada ya mkutano huo, mawaziri waliwataka Wataliban kuhakikisha "usalama" wa wageni na Waafghan wanaotaka kuondoka Afghanistan. Pia walisisitiza "hitaji la pande zote kuheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu".

Wiki moja baada ya Taliban kuchukua madaraka nchini Afghanistan, maelfu ya watu leo Jumapili wamekuwa wakijaribu kuitoroka nchi yao kwa kuhofia usalama wao wakati shughuli za uokoaji kutoka nchi za nje zikiendelea katika mazingira magumu. Raai saba wa Afghanistan walifariki dunia katika maziira yasiyoeleweka, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema Jumapili hii bila kutoa maelezo zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.