Pata taarifa kuu
EU-AFGHANISTAN

Afghanistan: EU yatoa wito kwa nchi wanachama kukubali kuwapokea wakimbizi

Pamoja na Mkuu wa Serikali ya Uhispania Pedro Sanchez, rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen na rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel wamezuru kituo cha mapokezi huko Torrejon de Ardoz, nchini Uhispania, ambapo ndege zinazoshiriki zoezi la uokoaji zinafika chache kutoka Afghanistan.

Ursula Von der Leyen, Charles Michel (kulia) na Pedro Sanchez huko katika kambi ya jeshi la wanamaji huko Torrejon karibu na Madrid, Agosti 21, 2021.
Ursula Von der Leyen, Charles Michel (kulia) na Pedro Sanchez huko katika kambi ya jeshi la wanamaji huko Torrejon karibu na Madrid, Agosti 21, 2021. REUTERS - JUAN MEDINA
Matangazo ya kibiashara

Mashariki mwa Madrid, uwanja wa ndege wa Torrejon de Ardoz umekuwa kituo cha mapokezi kwa raia wa Ulaya na pia kwa raia wa Afghanistan ambao wameshirikiana na taasisi za kimataifa. Ni kutoka kwa kituo hiki cha jeshi, nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya wataamuwa nchi gani watapelekwa Waafghani katika nchi mbalimbali za Umoja huo.

Wakati huo rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema umoja huo haulitambui kundi la Taliban na wala hautoshiriki mazungumzo ya kisiasa na kundi hilo. Matamshi ya Von der Leyen yamekuja wiki moja baada ya Taliban kuidhibiti Afghanistan ukiwemo.

Ursula von der Leyen amesema wako tayari kutoa msaada kwa Mataifa ya Ulaya ili kuwasaidia wakimbizi na pia amepanga kuwasilisha suala la makaazi kwa wakimbizi hao katika mkutano wa G7 wiki ijayo.

Kudorora kwa serikali ya Afghanistan kulianza wakati rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, alipokubali kuwaondoa wanajeshi wa Marekani nchini humo mpango ulioanza kutekelezwa miezi kadhaa mapema kuliko ilivyopangwa na rais wa sasa Joe Biden.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.