Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: Taliban yazindua mashambulizi makubwa dhidi ya waasi Panshir

Taliban, wanaoshikilia tena madaraka nchini Afghanistan tangu wiki moja iliyopita, siku ya Jumapili , Agosti 22, walitangaza kuzindua mashambulizi makubwa dhidi ya eneo pekee ambalo bado linawapinga: bonde la Panshir. Katika mkoa huu wa milima, upinzani unaendelea kujipanga chini ya maagizo ya mtoto wa Kamanda Massoud.

Taliban ilitangaza kwamba "mamia" ya wapiganaji wao walikuwa wakielekea bonde la Panshir. Hapa, wapiganaji wa Taliban walipigwa picha huko Ghazni, kusini magharibi mwa Kabul, Agosti 13, 2021.
Taliban ilitangaza kwamba "mamia" ya wapiganaji wao walikuwa wakielekea bonde la Panshir. Hapa, wapiganaji wa Taliban walipigwa picha huko Ghazni, kusini magharibi mwa Kabul, Agosti 13, 2021. AP - Gulabuddin Amiri
Matangazo ya kibiashara

Taliban walitangaza kwamba "mamia" ya wapiganaji wao walikuwa wakielekea Bonde la Panchir, kaskazini mashariki mwa Kabul, moja ya maeneo machache ya Afghanistan ambayo bado halihadhibitiwa na kundi la Taliban.

"Mamia ya mujahedin kutoka Falme za Kiislamu [jina jipya rasmi lililopewa na Taliban kwa Afghanistan] wanaelekea katika jimbo la Panshir ili kudhibiti eneo hilo, baada ya maafisa wa eneo hilo kukataa kulikabidhi kwa amani," Taliban wamesema kwenye ukurasa wao wa Twitter kwa Kiarabu.

Taliban iliingia Kabul mnamo Agosti 15 bila upinzani wowote, kufuatia masjhambulizi makubwa iliyoanzisha mwezi Mei baada ya kuanza kuondoka kwa majeshi ya Marekani na NATO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.