Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Taliban: Hatutatangaza serikali ikiwa bado kuna wanajeshi wa Marekani Afghanistan

Kundi la Taliban limesema kwamba halitotangaza serikali yake hadi pale Marekani itakapokamilisha kuviondoa vikosi vyake. Vyanzo viwili ndani ya kundi hilo vimelieleza shirika la habari la AFP kuwa uundaji wa serikali na baraza la mawaziri hauwezi kutangazwa ikiwa bado kuna wanajeshi wa Marekani. 

Waafghani wanapanda ndege ya kikosi cha Anga cha Marekani C-17 Globemaster III wakati wa zoezi la kuwaondoa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai, Afghanistan, Agosti 22, 2021.
Waafghani wanapanda ndege ya kikosi cha Anga cha Marekani C-17 Globemaster III wakati wa zoezi la kuwaondoa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai, Afghanistan, Agosti 22, 2021. via REUTERS - US AIR FORCE
Matangazo ya kibiashara

Marekani inasema inalenga kumaliza operesheni ya kuwaondoa raia wake na wale wa Afghanistan ambao maisha yao yapo hatarini kutoka mjini Kabul kufikia Agosti 31, licha ya viongozi wa mataifa G7 wakitarajiwa kuihimiza Marekani kuongeza muda wa kuwa nchini humo.

Wapiganaji wa Taliban wameonya kuwa hawataruhusu wanajeshi wa Marekani kuendelea kuwa nchini humo zaidi ya mwisho wa mwezi huu.

Katika hatua nyingine, Ufaransa inasema raia wake zaidi ya 100 wameondolewa nchini Afghanistan kwa kupîtia nchi ya Falme za Kiarabu.

Mbali na raia wake, Ufaransa pia imefanikiwa kuwaondoa raia wa Afganistan 1,300 mpaka sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.