Pata taarifa kuu
USALAMA-HAKI

Mauaji yaongezeka nchini Afrika Kusini

Afrika Kusini imerekodi karibu mauaji 84 kwa siku kati ya mwezi Oktoba na Desemba, ongezeko la zaidi kwa mwaka mmoja, polisi imetangaza siku ya Ijumaa, wakati uhalifu ni mada kuu katika mjadala wa kisiasa kabla ya uchaguzi ujao.

Afrika Kusini ina moja ya viwango vya juu zaidi vya mauaji ya kila mtu duniani wakati wa amani.
Afrika Kusini ina moja ya viwango vya juu zaidi vya mauaji ya kila mtu duniani wakati wa amani. © Shiraaz Mohamed / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Takwimu hizi zinaweza kuaibisha chama tawala, ANC, ambacho kimetawala nchi hiyo tangu kuja kwa demokrasia miaka 30 iliyopita na kinakabiliwa na uchaguzi mkuu mgumu, uliopangwa kufanyika kati ya mwezi Mei na Agosti.

Uhamiaji usiofuata utaratibu na uhalifu uliokithiri ni masuala muhimu ya kisiasa kuelekea uchaguzi huu, huku vyama vya upinzani vikishutumu kushindwa kwa serikali.

Afrika Kusini ina moja ya viwango vya juu zaidi vya mauaji ya kila mtu duniani wakati wa amani. Waziri wa Polisi, Bheki Cele, anayekabiliwa na ukosoaji mkubwa, amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Pretoria kwamba watu 7,710 waliuawa katika robo ya mwisho ya mwaka 2023. "Inasikitisha na inatia wasiwasi kuona kwamba idadi ya watu waliouawa katika kipindi hiki iliongezeka kwa 2.1%" ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha mwaka 2022, ameongeza.

Ubakaji ulipungua kidogo, kwa 1.7%, ikilinganishwa na robo sawa ya mwaka uliopita. "Kinachosumbua kwa sasa na kuhuzunisha ni kwamba ubakaji mwingi ulifanywa katika nyumba za wahanga", wahusika wakiwa "ama majirani, marafiki au wanafamilia", amebainisha Bw. Cele.

"Utekaji nyara kwa ajili ya fidia umekuwa shughuli yenye faida kubwa kwa uhalifu uliopangwa nchini Afrika Kusini," waziri huyo pia ameonya, akisisitiza azimio la polisi la kupambana dhidi ya janga hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.