Pata taarifa kuu

Hali ya usalama mashariki mwa DRC katikati mwa ziara ya Félix Thisekedi nchini Ujerumani

Rais wa DRCongo, Félix Thisekedi, anatarajiwa leo Jumapili hii, Aprili 28 nchini Ujerumani. Hatua fupi kabla ya kuwasili Paris kwa siku mbili za ziara rasmi. Huko Berlin, Félix Thisekedi atakula chakula cha jioni na Chansela Kansela Olaf Scholz. Katika ajenda ya mkutano huu ni hali ya usalama mashariki mwa DRC.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi (katikati), wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU), Februari 18, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi (katikati), wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU), Februari 18, 2024. AFP - MICHELE SPATARI
Matangazo ya kibiashara

Mgogoro wa usalama ni suala la kipaumbele kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na katika ziara hii barani Ulaya, Félix Tshisekedi atazungumzia suala hilo wakati wa mikutano yake na viongozi wa kisiasa nchini Ujerumani na Ufaransa. DRC inayaomba maataifa haya kuchukua msimamo wa wazi kuhusu mzozo kati ya vikosi vya serikali na kundi la M23 linaloungwa mkono na nchi jirani ya Rwanda.

Ujerumani imelaani mara kwa mara uungaji mkono wa Kigali kwa kundi la waasi huko Kivu Kaskazini katika miaka ya hivi karibuni. Mwezi Machi mwaka jana, wakati wa mahojiano mjini Kinshasa na Waziri wa Ulinzi, Jean-Pierre Bemba, balozi wa Ujerumani alikwenda mbali zaidi, akitaja uwepo wa majeshi ya Rwanda nchini DRC. "Ukiukaji wa uhuru", kulingana na Ingo Hebert.

Ujerumani, ambayo pia ina wasiwasi kuhusu mzozo wa kibinadamu katika eneo hilo, matokeo ya mzozo na watu wake zaidi ya milioni moja waliokimbia makazi katika mji wa Goma pekee. Balozi wa Ujerumani mjini Kinshasa pia alikuwa sehemu ya wajumbe wa mabalozi wa nchi za Magharibi waliotembelea mji mkuu wa mkoa huo katikati ya mwezi Aprili, kwa lengo la kutahadharisha kuhusu mahitaji ya kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.