Pata taarifa kuu

DRC yaishutumu Apple kwa kunufaika na uchimbaji madini haramu

Serikali ya DRC inashutumu kampuni ya Apple kwa kutumia madini "yaliyochimbwa kinyume cha sheria" katika bidhaa zake,madini ambayo yanatoka kwenye "migodi ya Kongo" ambapo "haki nyingi za binadamu zinakiukwa", kulingana na nyaraka ambazo shirika la habari la AFP limepata kopi.

Cobalt ni madini yenye thamani kubwa, ambayo hutumiwa katika utengenezaji wa betri za simu za mkononi, kompyuta na magari ya umeme. Picha hii ilipigwa nchini DRC, nchi inayoongoza kwa uzalishaji duniani (70% ya uzalishaji duniani).
Cobalt ni madini yenye thamani kubwa, ambayo hutumiwa katika utengenezaji wa betri za simu za mkononi, kompyuta na magari ya umeme. Picha hii ilipigwa nchini DRC, nchi inayoongoza kwa uzalishaji duniani (70% ya uzalishaji duniani). Lucien KAHOZI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mawakili waliopewa mamlaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), madini haya "husafirishwa kutoka DRC na hasa kwenda Rwanda, ambako husafishwa".

"Inaonekana kutoka kwenye faili" iliyowasilishwa na DRC "kwamba kampuni ya Apple inatumia madini ya kimkakati yaliyonunuliwa nchini Rwanda katika bidhaa zake," wanasema mawakili waliopewa jukumu la kuandaa notisi rasmi, wito kabla ya kuanzishwa kwa kesi za kisheria.

"Rwanda ni mhusika mkuu katika uchimbaji haramu wa madini na hasa uchimbaji wa bati na tantalum nchini DRC," wanasema mawakili hao. "Baada ya uchimbaji wao haramu, madini haya yanasafirishwa kwenda Rwanda, ambapo yanaunganishwa katika njia za kimataifa za ugavi," inasema notisi rasmi.

"Madini haya yanayozozaniwa yanatoka kwa kiasi kikubwa kwenye migodi ya Kongo ambapo haki nyingi za binadamu zinakiukwa," mawakili hao wanaongeza.

Notisi hii rasmi ilitumwa wiki hii kwa kampuni tanzu mbili za Apple nchini Ufaransa na mawakili wa Ufaransa William Bourdon na Vincent Brengarth. Barua pia ilitumwa kwa kampuni mama nchini Marekani, ambayo inauza sana iPhone na kompyuta aina ya Mac.

Ardhi ya DRC imejaa madini, nchi hiyo ikiwa inaongoza kwa uzalishaji wa cobalt na nchi hii inaongoza Afrika kwa uzalishaji wa shaba.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika lisilo la kiserikali la The Enough Project iliyochapishwa mwaka wa 2015, "maeneo haya ya madini mara nyingi yanaonekana kudhibitiwa na makundi yenye silaha ambayo hulazimisha, kupitia vurugu na ugaidi, raia kufanya kazi na kusafirisha madini haya. Watoto pia wanalazimika kufanya kazi katika migodi hii.

Serikali ya Kinshasa inaishutumu Rwanda kwa kutaka kuchukua udhibiti wa rasilimali, hususan madini, ya Wakongo wa mashariki, moja ya sababu kwa nini, kwa mujibu wake, Kigali inaunga mkono waasi wa M23, kwa mashambulizi ya zaidi ya miaka miwili katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

M23 kwa sasa inadhibiti sehemu kubwa ya mkoa wa Kivu Kaskazini na maeneo yanazunguka mji mkuu wa mkoa huo, Goma.

Notisi hii rasmi ya Apple inaelezwa, kulingana na wanasheria hawa, kuwa "na uzito wa ajabu wa hali ya mashariki mwa DRC na ambayo ni chanzo cha uharibifu mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo na taifa nzima la Kongo."

Wanasheria hao wanaona "haitoshi" "ahadi na tahadhari mbalimbali zilizochukuliwa" na Apple, "ama kwa hiari yake yenyewe au kwa kutumia sheria kuhusu matumizi ya madini yanayonunuliwa nchini Rwanda".

"DRC ina nia ya kuweka maadili katika sekta ya uchimbaji madini adimu, hasa yanapochimbwa kwa gharama ya kufanya uhalifu mkubwa na wakati mwingine kwa manufaa ya wale wanaotenda uhalifu," wanahoji.

Mnamo Aprili 2022, shirika lislo la kiserikali kutoka Uingereza la Global Witness lilishutumu mpango huu kwa kuchangia nchini DRC kinyume chake katika utoroshaji wa madini yanayohusishwa na migogoro, ajira ya watoto, au kutokana na biashara haramu na magendo.

Notisi rasmi ya Apple kutoka DRC inaambatana na orodha ya maswali kuhusu "madini ya 3T yanayotumika katika bidhaa za Apple". Wanasheria wanaitaka Apple kujibu "ndani ya wiki tatu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.