Pata taarifa kuu

TotalEnergies yalengwa na uchunguzi wa "mauaji" kwa shambulio la wanajihadi nchini Msumbiji

Kampuni kubwa ya hydrocarbon TotalEnergies kwa mara nyingine tena iko chini ya shinikizo la kisheria. Nchini Ufaransa, uchunguzi wa awali ulifunguliwa Jumamosi Mei 4 kwa "kuua bila kukusudia" na "kushindwa kumsaidia mtu aliye hatarini" dhidi ya TotalEnergies. Tukio hilo lilianza mwaka 2021, wakati wa shambulio la wanajihadi huko Palma nchini Msumbiji. Kampuni kubwa ya hydrocarbon, ambayo ilikuwa na mradi wa gesi katika eneo hilo, inashutumiwa kwa uzembe katika kutathmini hatari za usalama.

Maafisa wa polisi wa Rwanda wakitoa ulinzi kwenye eneo la mradi wa LNG ya TotalEner Msumbiji huko Afungi, jimbo la Cabo Delgado, Msumbiji, Septemba 29, 2022.
Maafisa wa polisi wa Rwanda wakitoa ulinzi kwenye eneo la mradi wa LNG ya TotalEner Msumbiji huko Afungi, jimbo la Cabo Delgado, Msumbiji, Septemba 29, 2022. © Camille Laffont / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi huu ni "hatua chanya mbele" kwa walalamikaji. Miongoni mwao ni waathiriwa wa shambulio la wanajihadi lililoanza mnamo Machi 24, 2021 huko Palma. Shambulio hilo lililodumu kwa siku kadhaa, lilidaiwa na kundi la Islamic State (IS). Maputo ina waathiriwa takriban thelathini pekee, lakini kulingana na uchunguzi wa tovuti wa mwandishi wa habari huru Alexander Perry, idadi ya vifo ni raia 1,402 waliokufa au kupotoweka, wakiwemo wakandarasi 55.

Wengi wao walikuwa wamekimbilia katika hoteli iliyo nje kidogo ya jiji, Amarula Lodge, iliyozingirwa kwa siku kadhaa na wanajihadi. Takriban watu saba waliuawa wakijaribu kutoroka.

Waathiriwa wanaolalamika huelekeza kwenye "sehemu ya wajibu" ya TotalEnergies katika shambulio hili kwa "kushindwa kumsaidia mtu aliye hatarini". Kwa sababu wanashutumu kampuni hii ya mafuta kwa kukataa kusaidia juhudi za kutoa msaada kwa kutoa mafuta kwa helikopta ambazo zilikuwa zikiondoa raia. Shtaka lingine: ukosefu wa ulinzi kwa wakandarasi wadogo. Walalamikaji hata hivyo wanahakikisha kwamba kampuni hiyo "ilifahamishwa juu ya uwezekano wa shambulio" na wanajihadi.

“Tunafurahi kwamba mwendesha-mashtaka wa Ufaransa aliitikia upesi kwa kutilia maanani maombi yetu,” amesema Nicholas Alexander, mlalamikaji kutoka Afrika Kusini ambaye alinusurika katika shambulio hilo.

Ripoti kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na makampuni ya ushauri pia yananyooshea kidole dosari katika mpango wa usalama wa kampuni hiyo.

Mradi wa dola bilioni 20 kwa Total katika eneo lililo katikati ya mapigano na Al Shabab

TotalEnergies, kwa mara nyingine tena chini ya makabiliano na mahakama, "inakataa mashtaka haya". Wakati wa kuwasilisha malalamiko mwaka jana, kampuni hiyo imekumbusha "msaada wa dharura uliohamasishwa na timu zake kuwezesha kuwahamisha watu 2,500" kutoka eneo la Afungi, karibu kilomita kumi kutoka Palma, katika mashambulizi ya kituo hicho.

Kwenye hili, eneo la ujenzi wa mradi mkubwa wa gesi ulikuwa unafanyika. Mradi huu wa uwekezaji wenye thamani ya dola bilioni 20 hadi sasa umesitishwa, lakini jumuiya ya kimataifa inatarajia kuuzindua upya, kulingana na Mkurugenzi Mtendaji wake Patrick Pouyanné.

Shambulio lililopangwa kwa uangalifu dhidi ya Palma, mji wa wakaazi 75,000, liliashiria kuongezeka kwa vita vya msituni vilivyoanzishwa mnamo mwaka 2017 na makundi ya wanajihadi, yanayojulikana kama Al Shabab. Mapigano hayo tangu wakati huo yamesababisha maelfu kadhaa kuuawa na mamia ya maelfu kuyahama makazi yao katika jimbo hili, Cabo Delgado, maskini lakini tajiri wa gesi asilia.

Tangu mwezi wa Julai 2021, maelfu ya wanajeshi kutoka Rwanda na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wametumwa kusaidia jeshi la Msumbiji, na kusaidia kurejesha udhibiti wa sehemu kubwa za Cabo Delgado.

Mashtaka mengine kadhaa dhidi ya Total

Uchunguzi huu ni pamoja na taratibu nyingine za kisheria ambazo TotalEnergies inahusishwa.

Mnamo mwezi Juni, Waganda 26 na mahirika walianzisha hatua za kiraia mjini Paris kudai "fidia" kwa uharibifu mbalimbali unaohusishwa na miradi mikubwa miwili katika Afrika Mashariki. Miongoni mwa uharibifu huu ni kunyang'anywa mali kwa njia mbaya, fidia isiyotosheleza na mengine.

Mashirika hayo, ikiwa ni pamoja na Muungano wa Darwin Climax na Sea Shepherd France, pia viliwasilisha malalamiko ya jinai mnamo Septemba 22 huko Nanterre kuhusu jukumu la hali ya hewa la TotalEnergies. Hii inalenga EACOP/Tilenga na kwa upana zaidi uwekezaji wake wa mafuta na gesi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.