Pata taarifa kuu

Chad: Zaidi ya wanajeshi 70 wa Marekani watahamishwa kutoka Ndjamena

Marekani inapanga kuwaondoa kwa muda baadhi ya wanajeshi wake kutoka Chad, maafisa wa Marekani wametangaza. Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya Washington kulazimika kukubali kuondoa wanajeshi wake katika nchi jirani ya Niger.

Wanajeshi wa Marekani katika kambi ya jeshi ya Grafenwöhr, Ujerumani.
Wanajeshi wa Marekani katika kambi ya jeshi ya Grafenwöhr, Ujerumani. AFP - CHRISTOF STACHE
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu Washington, Guillaume Naudin

Kuondoka huku kwa muda kunahusu idadi ndogo ya askari wa kikosi maalum cha Marekani, haswa wapangaji mipango na washauri waliopo nchini Chad kwa sasa. Wanajeshi hawa watatumwa tena Ujerumani katika hatua ya mwanzoni. Wanajeshi 75 ndi watahusika na mpango huo.

Msemaji wa Pentagon Jenerali Patrick Ryder amesema baadhi ya wanajeshi wa Marekani nchini Chad watatumwa tena nje ya nchi hiyo. Amesema ni "hatua ya muda" katika tathmini inayoendelea ya ushirikiano wa kiusalama na Chad, ambayo itaanza tena baada ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Mei 6.

Afisa wa Marekani, akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, amesema wanajeshi kadhaa wa kikosi maalum ambao wako nchini Chad kama wapangaji mipango na washauri watahamia Ujerumani kwa sasa.

Kuondolewa kwa wanajeshi hao ni sehemu ya hali tata iliyobainishwa na kusimamishwa kwa shughuli za Marekani kwenye kituo kikuu cha anga na mkuu wa majeshi ya jeshi la anga la Chad na kufanyika kwa uchaguzi muhimu wa urais nchini humo.

Mapema mwezi huu, mkuu wa jeshi la anga la Chad aliagiza Marekani kusimamisha shughuli katika kituo cha anga karibu na mji mkuu N'Djamena, kwa mujibu wa barua iliyotumwa kwa serikali ya mpito.

Katika barua hiyo ya tarehe 4 Aprili na kutumwa kwa Waziri wa Majeshi ya Chad, mkuu wa majeshi ya jeshi la anga, Idriss Amine Ahmed, anadai kumtaka afisa wa ulinzi wa Marekani kusimamisha shughuli za Marekani katika kituo cha anga cha Adji Kossei baada ya "Marekani" kuonekana kuwa haikutoa hati zinazohalalisha uwepo wao.

Athari ya kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani 

Chad imekuwa na jukumu kubwa kama mshirika wa vikosi vya Magharibi katika vita dhidi ya makundi ya jihadi huko Afrika Magharibi. Umuhimu wake wa kimkakati hauwezi kupuuzwa.

Kujiondoa kwa Marekani, ingawa ni kwa muda, kunaweza kuathiri juhudi za kukabiliana na ugaidi katika eneo hilo, hasa kwa vile Chad imekuwa mshirika muhimu katika mapambano hayo. Hali tete ya usalama katika Sahel pia inaweza kudhoofishwa zaidi, kukiwa na athari zinazowezekana kwa nchi jirani.

Athari za muda mrefu za uondoaji huu wa muda kwenye uhusiano kati ya Marekani na Chad bado zinapaswa kuamuliwa. Maafisa wa Marekani walisisitiza, hata hivyo, kwamba hii ni hatua ya muda na kwamba ushirikiano kati ya nchi hizo mbili bado ni imara.

Kuondoka kwa sehemu kwa wanajeshi wa Marekani nchini Chad ni sehemu ya mwelekeo mpana wa urekebishaji wa uwepo wa wanajeshi wa Marekani huko Afrika Magharibi, ili kukabiliana na mabadiliko ya kisiasa na changamoto za kiusalama katika eneo hilo.

Kuundwa upya kwa ushirikiano wa kijeshi na kutafuta mbinu mpya za kupambana na ugaidi na kukuza utulivu wa kikanda itakuwa masuala muhimu katika miezi na miaka ijayo.

Katika nchi jirani ya Niger, utawala wa kijeshi uliiomba Marekani kuwaondoa wanajeshi wake nchini humo kutokana na kutofautiana na Washington kuhusu masuala kama vile maendeleo katika kipindi cha mpito cha nchi hiyo kuelekea utawala wa kidemokrasia.

Marekani ilisema majadiliano yameanza kuhusu kuondoa majeshi nchini Niger, ambayo hadi mapinduzi ya mwaka jana ilikuwa mshirika mkuu katika mapambano ya Washington dhidi ya wanajihadi ambao wameua maelfu ya watu na mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.