Pata taarifa kuu

Rais Ramaphosa ameagiza kutumwa kwa wanajeshi 2900 nchini DR Congo

Nairobi – Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameagiza kutumwa kwa wanajeshi 2900 nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kusaidia mapambano dhidi ya makundi yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo, hatua hii ikienda sambamba na jukumu la nchi hiyo kuchangia wanajeshi katika jumuiya ya SADC pamoja na kuisaidia DRC.

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameagiza kutumwa kwa wanajeshi 2900 nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameagiza kutumwa kwa wanajeshi 2900 nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo AP
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao watakuwa kama sehemu ya ujumbe wa kusini mwa Afrika nchini DR Congo (SAMIDRC), ambao uliidhinishwa na  uongozi wa kikanda mwezi Mei mwaka jana.

Malawi na Tanzania pia zitachangia wanajeshi wake katika ujumbe huo.

Ujumbe huo unachukua nafasi ya kikosi cha kanda ya Afrika Mashariki, ambacho kiliondoka DR Congo Desemba mwaka jana baada ya Kinshasa kudai kuwa kilikuwa kimeshindwa kutekeleza majukumu yake kama ilivyotakiwa.

Kikosi cha EAC kutoka Kenya, kikiondoka kwenye uwanja wa ndege wa Goma.21/12/2023
Kikosi cha EAC kutoka Kenya, kikiondoka kwenye uwanja wa ndege wa Goma.21/12/2023 © Chube Ngorombi, Goma

Tangazo hilo linakuja wakati huu mapigano mapya yakiripotiwa mashariki mwa nchi ya DRC kati ya wanajeshi wa serikali na makundi ya waasi.

Makumi ya maelfu ya raia wamelazimika kuyahama  makazi yao kutokana na vita vinayoendelea.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.