Pata taarifa kuu

Afrika Kusini yawasilisha madai mapya dhidi ya Israel mbele ya ICJ

Pretoria imetangaza Jumanne kwamba imewasilisha rufaa mpya kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) huko Hague ili kuchunguza kwa haraka tangazo la Israel la mashambulizi ya kijeshi yanayokuja dhidi ya Rafah na kupinga ikibidi "ukiukaji mpya wa haki."

Wajumbe wa Mahakama wakiwa katika ufunguzi wa kesi.
Wajumbe wa Mahakama wakiwa katika ufunguzi wa kesi. International Court of Justice (ICJ)
Matangazo ya kibiashara

 

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu hivi karibuni aliagiza jeshi lake kuandaa mashambulizi katika mji wa Rafah, kimbilio la mwisho la Wapalestina milioni 1.4, kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya nusu ya jumla ya wakazi wa eneo hilo, wengi wao wakiwa wamekimbia vita ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa miezi minne. Shinikizo la kimataifa tangu wakati huo limeongezeka kwa makubaliano ya usitishaji vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas.

Pretoria ilisema kuwa imewasilisha rufaa ya dharura kwa ICJ siku ya Jumatatu. Afrika Kusini tayari imepeleka suala hilo kwenye mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa, ikiishutumu Israel kwa "mauaji ya halaiki" huko Gaza. Majaji, ambao hawakusema lolote wakati huu kuhusu suala la iwapo Israel inatekeleza mauaji ya halaiki au la, hata hivyo waliiamuru kuzuia vitendo hivyo.

Katika rufaa yake mpya, Pretoria imesema "ina wasiwasi mkubwa" na "mauaji, majeraha na uharibifu mkubwa" ambao unaweza kusababishwa na operesheni ya Israel huko Rafah. Kulingana na serikali ya Afrika Kusini, hii "itajumuisha ukiukaji mkubwa na usioweza kurekebishwa wa Mkataba wa Mauaji ya Kimbari." ICJ, ambayo haitakiwi kushughulikia kesi hiyo, haijathibitisha katika hatua hii kwamba imepokea faili. Maamuzi ya Mahakama ni ya lazima na hayawezi kupingwa kwa kukata rufaa, lakini haina njia ya kutekeleza maamuzi yake.

Vita hivyo vilichochewa Oktoba 7 na shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa na makomando wa Hamas waliojipenyeza kutoka Ukanda wa Gaza hadi kusini mwa Israel, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,160, raia walio wengi waliuawa siku hiyo, kulingana na hesabu ya shirika la habari la AFP likijikita kwa data za Israeli.

Katika kulipiza kisasi, serikali ya Israel iliapa kuiangamiza Hamas, ambayo imekuwa madarakani katika Ukanda wa Gaza tangu mwaka 2007. Zaidi ya watu 28,000 wameuawa tangu kuanza kwa vita katika eneo la Palestina, idadi kubwa ya raia, kulingana na Wizara ya Afya ya serikali ya Hamas. Kulingana na Israel, mateka 130 bado wako Gaza, 29 kati yao wanaaminika kufariki, kati ya karibu watu 250 waliotekwa nyara Oktoba 7. Makubaliano ya wiki moja mwezi Novemba yaliruhusu kuachiliwa kwa mateka 105 kwa kubadilishana na Wapalestina 240 waliokuwa wanazuiliwa na Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.