Pata taarifa kuu

Saudi Arabia yatoa wito kwa Israel 'kuwajibikia' kwa 'ukiukaji' wa sheria za kimataifa

Saudi Arabia siku ya Ijumaa imekaribisha uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu Israel, ikitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa "kuiwajibisha Israel" kwa "ukiukaji wake" wa sheria za kimataifa.

Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wakitoa uamuzi wao kuhusu Israel, huko Hague, Uholanzi, Januari 26, 2024.
Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wakitoa uamuzi wao kuhusu Israel, huko Hague, Uholanzi, Januari 26, 2024. © PIROSCHKA VAN DE WOUW / Reuters
Matangazo ya kibiashara

 

Katika taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Saudi Arabia pia imetoa wito wa "hatua zaidi" kufikia "kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza" na kutoa "ulinzi kwa raia wa Palestina".

Katika uamuzi uliotarajiwa sana, mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa imetoa wito siku ya Ijumaa Januari 26 kwa Israel kufanya kila linalowezekana kuzuia kitendo chochote cha "mauaji ya kimbari" katika Ukanda wa Gaza na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia.

Katika hatua hii ya kesi, ICJ pia haijatoa uamuzi wazi juu ya suala la madai ya mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza. Lakini hata hivyo inaona kuwa ni vitendo kama hivyo vinaweza kufanywa, anabaini mwandishi wetu huko The Hague, Stéphanie Maupas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.