Pata taarifa kuu

Viboko kadhaa wakwama kutokana na ukame nchini Botswana

Wakiwa wamenaswa kwenye matope ya madimbwi yaliyokauka, mamalia wakubwa wana hatari ya kufa: nchini Botswana, kundi zima la viboko ni wahanga wa ukame mkali, huku mamlaka za uhifadhi bado zikijaribu kurekodi hasara, wameliambia shirika la habari la AFP.

Mwonekano huu wa angani unaonyesha viboko wakiwa wamekwama kwenye mfereji mkavu karibu na kijiji cha Nxaraga kwenye Delta ya Okavango, viunga vya Maun, Aprili 25, 2024.
Mwonekano huu wa angani unaonyesha viboko wakiwa wamekwama kwenye mfereji mkavu karibu na kijiji cha Nxaraga kwenye Delta ya Okavango, viunga vya Maun, Aprili 25, 2024. © Monirul Bhuiyan / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Mifumo ya mito inakauka na wanyama wako hatarini," amesema Lesego Moseki, msemaji wa Idara ya Wanyamapori na Mbuga za Kitaifa (DWNP) huko Gaborone. "Kiboko wa Namiland wanategemea maji ya Delta ya Okavango," ameoongeza, akibaini kwamba idadi ya wanyama ambao wamekabiliwa na ukame bado haijajulikana.

Kusini mwa Afrika kumekumbwa na ukame mkubwa, unaoathiri mavuno mengi na kuwatumbukiza mamilioni ya watu kwenye njaa. Hivi karibuni nchi kadhaa katika eneo hilo zilitangaza hali ya maafa ya kitaifa. Kulingana na wataalamu, jambo hilo linatokana zaidi na mfumo wa hali ya hewa uiitwa El Niño, ambayo husababisha ongezeko la joto duniani.

Kaskazini mwa Botswana, karibu na eneo oevu kubwa la Okavango Delta, kukauka kwa Mto Thamalakane kumelazimu makundi ya viboko kwenye hifadhi za maji asilia karibu na mji wa kitalii wa Maun, ambapo watalii wengi hutembelea kwa kutalii katika mbuga kubwa za wanyamapori nchini humo.

Viboko wenye ngozi nene lakini nyeti wanahitaji kuoga mara kwa mara ili kuepuka kuchomwa na jua na kwa kawaida huishi katika maeneo yenye unyevunyevu. Kwa kukosa maji, wanaweza kuwa wa kali na kukaribia vijiji. Mamlaka za eneo zinaomba viboko hao wahamishwe hadi kwenye hifadhi, haswa ili kuepusha migogoro na binadamu.

Botswana ina mojawapo ya idadi kubwa zaidi ya viboko mwitu duniani, wanaokadiriwa na Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN) kati ya vielelezo 2,000 na 4,000. Aina hiyo inachukuliwa kuwa katika hatari kubwa ya kutoweka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.