Pata taarifa kuu

Côte d’Ivoire kuunga mkono kurejea kwa hiari kwa zaidi ya wakimbizi 55,000 wa Burkina Faso

Mwishoni mwa mkutano wa tatu wa Kamati ya Uratibu unaohusiana na usimamizi wa wakimbizi Kaskazini, ambao ulifanyika Jumatano Aprili 24, mamlaka ilianzisha majadiliano ili kuweka masharti ya kurejea kwa wakimbizi nchini mwao. Kulingana na makadirio ya hivi punde ya UNHCR, kuna karibu wakimbizi 55,000 wa Burkina Faso nchini Côte d’Ivoire.

Wakimbizi wa Burkina Faso nchini  Côte d'Ivoire.
Wakimbizi wa Burkina Faso nchini Côte d'Ivoire. PHILIPPE DESMAZES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Abidjan, Bineta Diagne

Kulingana na taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani, "hakuna mpango wa kuwarejesha wakimbizi makwao ulijadiliwa" wakati wa mkutano kuhusu suala la usimamizi wa wakimbizi Kaskazini, ambao ulileta pamoja mamlaka, wanadiplomasia na mashirika ya kiutu, siku ya Jumatano.

Kwa mujibu wa taarifa hii kwa vyombo vya habari, timu ya kiufundi inapaswa kuundwa wiki ijayo ili kutathmini mahitaji: "kutafakari kwa upande mmoja juu ya masharti ya msaada wa haraka kwa wakimbizi, na kwa upande mwingine, juu ya mchakato wa kutia moyo kurudi tena kwa wakimbizi hao nchini Burkina Faso”.

"Hali ni mbaya"

Tangu mwisho wa mwezi wa Julai, baadhi ya wakimbizi waliotambuliwa na kusajiliwa na mamlaka na UNHCR wamehifadhiwa katika maeneo mawili: huko Niornigue na Timalah, katika maeneo ya Tchologo na Boukani. Maeneo haya mawili yana wakimbizi hadi 12,000. Kwa sasa wamejaa. Wakimbizi wengi wamepewa hifadhi katika familia katika vijiji vilivyo karibu na mpaka.

"Hali ni mbaya," anasema Fidèle Sarassoro, katibu mtendaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa, aliyehojiwa na RTI. Waziri huyu anabainisha kuwa tafakari ilifanywa na washirika wa kigeni, ili wakimbizi "waweze kurejea katika nchi yao haraka iwezekanavyo".

"Wengi wao," anaongeza, "wanaamua kurudi kwa kutumiauwezo wao ... Na kwa hivyo huu ni uthibitisho kwamba wakimbizi hawa wanataka kurejea kwao. Tunapaswa kuwa na uwezo wa kuunda mazingira kwa hili, "anaeleza waziri, ambaye ni katibu mtendaji wa CNS.

Lakini tangazo hili linazua shaka fulani: “je Burkina Fasoiko salama vya kutosha kuruhusu wakimbizi kurejea nyumbani? ", anauliza mmoja wa maafisa mashirika ya kiutu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.