Pata taarifa kuu

Niger: Bintiye rais wa zamani Bazoum amshutumu Mahamadou Issoufou kuhusika na mapinduzi

Hinda Bazoum almemshutumu mtangulizi wa babake kama mkuu wa nchi, Mahamadou Issoufou, Ijumaa Aprili 27 kuwa "mhusika mkuu" wa mapinduzi ya kijeshi yaliyompindua babake mwishoni mwa mwezi Julai 2023. Hii ni mara ya kwanza kwa mtu wa karibu na rais wa zamani Bazoum kutoa shutuma kama hizo.

Rais wa zamani Mohamed Bazoum Mei 2022.
Rais wa zamani Mohamed Bazoum Mei 2022. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kanda, Serge Daniel

Katika makala iliyochapishwa na vyombo vya habari vya Niger, Hinda Bazoum anathibitisha kwamba baada ya mapinduzi yaliyompindua babake, "jambo gumu zaidi kukubali lilikuwa kugundua kwamba Mahamadou Issoufou ndiye alikuwa mhusika mkuu aliyepanga kila kitu". Kulingana na Hinda Bazoum, mtangulizi wa Mohamed Bazoum, kama rais wa Niger alikuwa na mkakati: "kulinda masilahi yake binafsi", na mapinduzi yalikuwa kumruhusu kurejea madarakani, baada ya kipindi kifupi cha mpito cha kijeshi ambapo Katiba mpya ingepitishwa.

Kwa maneno ya binti Mohamed Bazoum, kuna huzuni. Anakumbusha kwamba baba yake amekuwa na urafiki kwa miaka 33 na rais wa zamani Mahamadou Issoufou, lakini hatimaye alisalitiwa kwa njia ya "isiyofaa na ukatili".

Pia akiwa na hasira, Hinda Bazoum anashutumu mazingira ambamo anazuiliwa babake kwa miezi tisa na kuibua kile anachokiita "ugunduzi wa hivi punde" wa rais wa zamani Mahamadou Issoufou: "kuwasilisha ombi kwa mahakama mpya ya serikali ili kuomba kuvuliwa kinga baba yetu, kisha kuhukumiwa kwake na mahakama ya kijeshi. Lengo kulingana na bintiye Bazoum, kumfanya Mohamed Bazoum mtu asiyefaa. Baada ya shutuma zote hizi, Mahamadou Issoufou bado hajajibu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.