Pata taarifa kuu

Niger: Mahakama yaagiza kuachiliwa kwa ndugu wawili wa Mohamed Bazoum

Mahakama nchini Niger siku ya Jumanne Aprili 2 iiliagiza kuachiliwa kwa Abdourahamane Ben Hamaye, mwandishi wa habari ambaye alifanya kazi katika ofisi ya rais chini ya utawala wa Mohamed Bazoum na Mohamed Mbarek, binamu wa mke wa rais wa zamani.

Moja ya mitaa ya Niamey, Niger, Agosti 2, 2023. (Picha ya kielelezo).
Moja ya mitaa ya Niamey, Niger, Agosti 2, 2023. (Picha ya kielelezo). REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Watu hao wawili walikamatwa nchini Niger mwaka jana wakati wa jaribio la kutoroka la Rais wa zamani wa Niger Mohamed Bazoum. Wakishtakiwa kwa kula njama dhidi ya mamlaka, Abdourahamane Ben Hamaye na Mohamed Mbarek walikuwa bado chini ya ulinzi wa polisi karibu miezi 6 baada ya kukamatwa.

Hali ambayo jaji wa mahakama ilimfanya siku ya Jumanne Aprili 2 kwa kuagiza waachiliwe huru.

"Wateja wetu walikamatwa Oktoba 19 na Novemba 7 mtawalia na, hadi sasa, hawajafikishwa mbele ya mahakama. Hata hivyo, sheria kuhusu suala hilo husema waziwazi kwamba kizuizini chao, kwa sababu wako chini ya ulinzi wa polisi, hakipaswi kuzidi kipindi cha juu cha mwezi mmoja,” amesema mmoja wa mawakili wao, Maître Ibrahim Djibo.

“Wanatuhumiwa kwa makosa makubwa sana, ya kupanga njama dhidi ya mamlaka ya nchi. Na licha ya kila kitu, hadi sasa, hawajafikishwa mahakamani, wako mikononi mwa jeshi, bila kusema mikononi mwa CNSP, kwa sababu jeshi hutekeleza maagizo ya CNSP. Ikiwa jaji leo ​​atagiza waachiliwe, watakuwa wametendewa haki, inatakiwa tu kusoma sheria, na tumeridhika sana na jaji huyu ambaye alivunja ukimya na kuiambia mamlaka: heshimu sheria, kwa kuagiza kuachiliwa kwa watuhumiwa,” mmoja wa mawakili wa watuhumiwa amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.