Pata taarifa kuu

Tiani azungumza na Putin 'kuimarisha' ushirikiano kati ya Urusi na Niger

Mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Niger, Jenerali Abdourahamane Tiani, amezungumza kwa simu siku ya Jumanne na Rais wa Urusi Vladimir Putin kujadili hasa "kuimarishwa" kwa ushirikiano wao wa kiusalama, inabainisha taarifa rasmi kwa vyombo vya habari vya Niger.

Jenerali Tiani, ambaye anaongoza Niger tangu kupinduliwa kwa Rais wa kiraia Mohamed Bazoum mwezi Julai mwaka uliyopita, ameelezea "shukrani zake kwa msaada" wa Urusi iliyotoa kwa Niger na "mapambano" ya nchi hii ya Saheli kwa "uhuru", kulingana chanzo hicho.
Jenerali Tiani, ambaye anaongoza Niger tangu kupinduliwa kwa Rais wa kiraia Mohamed Bazoum mwezi Julai mwaka uliyopita, ameelezea "shukrani zake kwa msaada" wa Urusi iliyotoa kwa Niger na "mapambano" ya nchi hii ya Saheli kwa "uhuru", kulingana chanzo hicho. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Wakuu hao wawili wa nchi" walijadili haja ya kuimarisha ushirikiano wa kiusalama" kati ya Urusi na Niger "kukabiliana na vitisho vya sasa", inabainisha taarifa kwa vyombo vya habari iliyosomwa kwenye redio ya umma ya Niger, wakati mashambulizi ya wanajihadi yanadhoofisha kanda ya Sahel. Jenerali Tiani, ambaye anaongoza Niger tangu kupinduliwa kwa Rais wa kiraia Mohamed Bazoum mwezi Julai mwaka uliyopita, ameelezea "shukrani zake kwa msaada" wa Urusi iliyotoa kwa Niger na "mapambano" ya nchi hii ya Saheli kwa "uhuru", kulingana chanzo hicho.

Taarifa ya Kremlin imesema pande hizo mbili zimeeleza "utayari wao wa kufufua mazungumzo ya kisiasa na kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana katika maeneo mbalimbali." "Mabadilishano ya maoni juu ya hali katika eneo la Sahara na Sahel pia yalifanyika, kwa msisitizo juu ya uratibu wa hatua za kuhakikisha usalama na mapambano dhidi ya ugaidi," Moscow imesema.

Mkutano huo umefanyika, kwa upande wa Niger, mbele ya Waziri Mkuu Ali Mahaman Lamine Zeine, Waziri wa Ulinzi, Jenerali Salifou Mody na wa Mambo ya Ndani, Jenerali Mohamed Toumba, kulingana na taarifa ya vyombo vya habari ya Niger. Katikati ya mwezi Machi, Niger ilishutumu makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Marekani, ikitilia shaka uwepo wa zaidi ya wanajeshi 1,000 wa Marekani nchini Niger.

Niger, kama nchi jirani za Burkina Faso na Mali, imekuwa ikikabiliwa na ghasia za wanajihadi za mara kwa mara na mbaya kwa miaka mingi, zinazofanywa na makundi ya wanajihadi yenye mafungamano na Al-Qaeda na Islamic State. Katika nchi hizi tatu, serikali za kiraia zimepinduliwa na mapinduzi ya kijeshi mfululizo tangu mwaka 2020.

Kwa kuongezea, makoloni haya matatu ya zamani ya Ufaransa yaliipa kisogo Paris na kusogea karibu zaidi kiuchumi na kijeshi na washirika wapya, ikiwa ni pamoja na Urusi, kabla ya kujipanga upya ndani ya Muungano wa Nchi za Sahel (AES) kwa lengo la kuunda shirikisho.

Katikati ya mwezi wa Januari, Urusi ilikuwa tayari imetangaza kwamba imekubali "kuimarisha" ushirikiano wake wa kijeshi na Niger. Ujumbe wa Urusi ulikwenda Niamey mnamo mwezi wa Desemba kujadili na jeshi. Makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa kijeshi yalitiwa saini. Niger, Burkina Faso na Mali zilitangaza mwishoni mwa mwezi wa Januari kwamba wanaondoka katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) na kuanzisha kikosi cha pamoja dhidi ya makundi ya kijihadi.

Mkutano huu kati ya Rais Putin na Jenerali Tiani unakuja siku nne baada ya shambulio dhidi ya ukumbi wa tamasha katika viunga vya jiji la Moscow, lililodaiwa na Islamic State na kusababisha vifo vya takriban watu 139.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.